Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Syria wanaoingia Iraq wamezidi 10,000-UNHCR

Syria, jimbo la Al-Hasakeh Oktoba 11, 2019, wanawake waliofurushwa wakisafiri kwa njia ya bara bara.
WFP/Alan Ali
Syria, jimbo la Al-Hasakeh Oktoba 11, 2019, wanawake waliofurushwa wakisafiri kwa njia ya bara bara.

Wakimbizi wa Syria wanaoingia Iraq wamezidi 10,000-UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Timu ya wahudumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyoko Kaskazini mwa Iraq imeripoti kwamba jana usiku wakimbizi zaidi ya 900 kutoka Syria wamewasili katika kambi ya Bardarash kwa kutumia mabasi 45 na kufanya idadi ya wakimbizi katika kambi hiyo kufikia 9,700.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic mjini Geneva Uswis hii leo, sasa jumla ya wakimbizi walitoka Syria na kuingia Iraq ni Zaidi ya 10,100 wakisaka usalama. “Karibu asilimia 75 ya wakimbizi wote walioandikishwa ni wanawake na watoto na zaidi ya robo ya familia za wakimbizi ni zinaendeshwa na wanawake na watu wanaowasili wanajumuisha pia watoto walio peke yao bila wazazi ama walezi.”

Hivi sasa UNHCR na washirika wao wanaendelea kutoa msaada wa kuokoa maisha . Timu ya kiufundi uya UNHCR, ya ulinzi na uandikishaji wa wakimbizi pamoja na washirika wengine kambini hapo kila siku wanatathimini na kukidhi mahitaji ya msingi mapema iwezekanavyo na pia wanahakikisha kwamba huduma zote kambini zinapatikana  na wakimbizi wapya wanaowasili wanashughulikiwa mara moja na kupewa msaada na huduma za muhimu.

Uhuru kwa wakimbizi

UNHCR inasisitiza umuhimu wa uhuru wa kutembea kwa raia wanaokimbia vita na kwamba mpka unapaswa kusalia wazi ili wakimbizi waweze kuingia kusalama usalama na ulinzi. Shirika hilo na wadau wengine wanashirikiana kwa karibu na uongozi wa jimbo la Kurdistan nchini Iraq (KRI) na wamedhamiria kusaidia kukabiliana na waimbi kubwa la wakimbizi wanaomiminika jimboni humo kutoka Syria hivi sasa.

Wakimbizi wengi wapya wanaowasili wanahitaji msaada wa kisaikolojia  watoto na watu wazima. Kama sehemu ya msaada wa pamoja wa mashirika mbalimbali UNHCR inatoa usaidizi na huduma za ulinzi kwa maelfu ya watu ili kuhakikisha usalama na utu haraka iwezekanavyo kwa watu wenye ulemavu ambao wametawanywa. UNHCR inakadiria kwamba fedha zaidi inazozihitaji kwa ajili ya mahitaji ndani ya Syria n idola milioni 31.5.