Ushirikiano baina ya vyuo vikuu utasaidia kuinua elimu Afrika- Profesa Miyamueni
Ushirikiano baina ya vyuo vikuu utasaidia kuinua elimu Afrika- Profesa Miyamueni
Jukwaa la kimataifa la vyuo vikuu barani Afrika na ughaibuni kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na mustakabali wa elimu katika bara hilo, limezinduliwa rasmi kwenye makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.
Akizungumza na UN News Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa mkutano huo, Profesa Antoine Kiamiantako Miyamueni, mdadhiri wa masuala ya uchumi katika chuo kikuu cha Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC) amesema mkutano huo ni muhimu katika maendeleo ya elimu ya vyuo vikuu nchini DRC na barani Afrika kwa kuwa unajikita na changamoto zinazokabili bara la Afrika katika sekta ya elimu.
(Sauti ya Profesa Miyamueni)
Nchini zetu na vyuo vyetu vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa utaalamu. Tunatarajia kwamba katika mkutano huu tutaweza kutengeneza ushirikiano baina ya vyuo vyetu pamoja na vyuo vikuu vya nchi zilizoendelea kaskazini .
Na kuhusu changamoto zinazokabili sekta ya elimu DRC amesma
(Sauti ya Profesa Miyamueni)
Elimu nchini kwetu iko katika viwango duni sana kwasababu walimu hawafundishi ipasavyo kwa ukosefu wa mishahara na motisha. Matokeo yake ni kwamba wanafunzi wanaojiunga na chuo kikuu wanakosa elimu bora.
Profesa Miyamueni ameota wito wa mshikamano wa nchi za Kiafrika katika sekta ya elimu ili kuboresha mustakabali wa elimu kwa ajili ya vizazi vijavyo.