UN yaeleza kutiwa wasiwasi na matamshi ya Netanyahu

12 Septemba 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea kutiwa wasiwasi na taarifa ya waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kuhusu mipango yake ya kutaka kunyakua bonde la Jordan na kaskazini mwa bahari ya chumvi endapo atachaguliwa, kama hatua ya kwanza ya kuonyesha mamlaka yake ya  utawala kwa makazi na maeneo mengine yanayokaliwa kwenye ukingo wa magharibi.

Taarifa ya Katibu Mkuu iliyotolewa kupitia msemaji wake imemnukuu akisema iwapo hatua hizo zitatekelezwa, hiyo itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Itakuwa ni pigo kubwa kwa hatu za kuanzisha upya majadiliano na amani ya kanda hiyo huku ikitishia uwezekano wa suluhu ya mataifa mawili.

Taarifa ya Katibu Mkuu imesema Umoja wa Mataifa unaendelea na dhamira yake ya kusaidia wapalestina na waisraeli kutatu mzozo wao katika msingi wa maazimio husika ya Umoja huo, mapendekezo ya  Madrid, ikiwemo muongozo wa ardhi kwa ajili ya maani, mradi wa amani wa waaraby na muongozo wa pande nne pamoja na kwa mujibu wa makubaliano ya awali ya serikali ya Israeli na shirika la Palestina la uhuru na kufikia maono ya mataifa mawili Israeli na taifa huru, la kidmokrasia ;a Palestina wakiishi upande mmoja na lingiine kwa amani na usalama katika mipaka inayotambuliwa kwa misingi ya mipaka ya kabla yam waka 1967.

Mtaalam wa UN asema unyakuaji huo unahatarisha suluhu ya mataifa mawili.

Kwa upande wake mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa hali ya haki za binadamu katika maeneo yanayokaliwa ya Palestina Michael Lynk amesema,“kutangaza haki ya kutaka kunyakua katika karne ya 21 ni kujaribu kuingia katika Dunia ambayo haipo tena. Ameongeza kwamba., “unyakuaji haukubaliki chini ya sheria ya kimatifa na chini ya mazingira yoyote, isitoshe kwa ajili ya sababu za kisiasa au kiuchaguzi.

Bwana Lynk amesema unyakuaji ulifanywa kuwa makosa na jamii ya kimatifa mwaka 1945 wakati wa kuridhia mkataba wa  kuanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945.

Mtaalam huyo maalum ametoa wito kwa jamii ya kimatifa kuenda mbali zaidi ya kutoa tu maneno ya kulaani unyakuaji huo akisema, “Kukashifu bila kuwajibisha hakuwezi kuhalalishwa katika mzozo huu, kuendelea kukaliwa kwa maeneo hayo hakutakufa kwa uzee. Ni kwa kuweka mikakati ya kupinga ukaliaji huo usio halali ambapo kuna fursa ya kupindua ahadi hii ya kunayaku na hatimaye kumaliza ukaliaji huo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud