Guterres ashtushwa na vifo vilivyotokana na mafuriko Jordan

26 Oktoba 2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amestushwa na vifo na uharibifu uliosababnishwa na mafuriko makubwa nchini Jordan ambayo yamearifiwa pia kusomba basi lililokuwa limebeba waalimu na wanafunzi waliokuwa katika safari ya shule.

Duru za habari zinasema takriban watu 18 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. Waathirika walisombwa na maji ya mafuriko hayo katika eneo la chemichemi la Zara Maeen kwenye bonde la bahari ya chumvi kufuatia mvua kubwa zilizonyesha siku ya Alhamisi.

Majeruhi wengi hivi sasa wanapatiwa matibabu na operesheni ya uokozi inaendelea.

Bwana. Guterres ametuma salam za rambirani kwa familia za waathirika na serikali ya Joridan.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia operesheni za uokozi na misaada. Bonde la bahari ya chumvi nchini Jordan limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na kwamba liko chini ya usawa wa baharí na mafuriko hutokea maji ya mvua yanapoanza kutiririka kutoka milimani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter