WMO yaanzisha mradi wa kuokoa maisha dhidi ya athari za hali ya hewa ziwa Victoria
WMO yaanzisha mradi wa kuokoa maisha dhidi ya athari za hali ya hewa ziwa Victoria
Maelfu ya watu hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kutopata tahadhari ya mapema ya majanga yatokanayo na hali ya hewa kama vimbunga, mafuriko, na hata matetemeko ya ardhi. Ili kuokoa maisha shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO sasa linachukua hatua likishirikiana na nchi mbalimbali kuhakikisha tahadhari inachukuliwa mapema.
Katika ziwa Victoria, Afrika Mashariki shirika hilo la WMO imezindua mradi ujulikanao kama “HIGHWAY “ mradi ambao ni mfumo wa kisasa wa hali ya juu wa kutoa tahadhari kwa lengo la kuokoa maisha hasa ya wavuvi na wasafiri wanaotumia ziwa hilo. Seleman Salim Said ni mvuvi wa ziwa Victoria kutoka eneo la Kayenze Mwanza nchini Tanzania
(SAUTI YA SELEMAN SALIM SAID)
Kwa bahati mbaya kila mwaka maelfu ya wavuvi hupoteza maisha kutokana na kutokuwa na mfumo wa kutoa tahadhari ya hali ya hewa ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa kabisa la uvuvi duniani linalozalisha mamilioni ya tani za samaki kila mwaka zinazoingiza dola milioni 600 kwa mwaka lakini athari zake kwa watu ni kubwa hivyo WMO ikaanzisha mradi wa HIGHWAY kushughilkia changamoto hii mradi ambao unajumuisha wadau wa kimataifa, kitaifa na kikanda zikiwemo ofisi za utabiri wa hali ya hewa za Kenya, Rwanda,Tanzania na Uganda, Uingereza naJumuiya ya Afrika Mashariki . Joseph Omer ni mvuvi jijini Jinja nchini Uganda
(SAUTI YA JOSEPH OMER)
Naye Samwel Osewe mwenyekiti wa fukwe ya Kiumba Kisumu, Kenya anasema
(SAUTI YA SAMWEL OSEWE)
“Nadhani tunaweza kutumia mfumo ambao mafunzo yanatolewa kwa jamii na mabaraza ya vijiji yanaitwa na wataalam wa utabiri wa hali ya hewa wakatoa tarifa kwa umma kuhusu hali ya hewa itakuwaje, kwani tunapokwenda ziwani tunategemea htu hali ya hewa.”
Kupitia mradi wa HIGHWAY mafunzo yatatolewa kuimarisha utoaji tahadhari mapema kuhusu hali ya hewa kupitia redio na simu za rununu. Lengo kuu l;a mradi ni kujenga mnepo na kuepusha vifo.