Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame, Kimbunga na mabadiliko ya kiuchumi yanaathiri hali ya kibinadamu Zimbabwe- Parajuli

Bishow Parajuli, Mratibu Mkazi wa UN nchini Zimbabwe wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, (23 Agosti 2019)
UN Photo/ Assumpta Massoi
Bishow Parajuli, Mratibu Mkazi wa UN nchini Zimbabwe wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, (23 Agosti 2019)

Ukame, Kimbunga na mabadiliko ya kiuchumi yanaathiri hali ya kibinadamu Zimbabwe- Parajuli

Msaada wa Kibinadamu

Hali ya kibinadamu nchini Zimbabawe inaathriwa na mambo matatu: ukame, kimbunga na hatua za serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi na uhakika wa chakula unasonga kutoka janga hadi hali ya dharura kwas asa idadi ya watu walio na mahitaji ikiwa ni milioni tano na idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa hapa makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe, Bishow Parajuli amesema hali ya kibinadamu ni mbaya wakati huu ufuatiliaji wa wakazi mijini ukiendelea kutafiti mahitaji yao ambapo nusu ya watu wote nchini Zimbabwe huenda wakahitaji msaada wa kibinadamu kwa njia moja au nyingine ikiwemo;

(Sauti ya Parajuli)

“Chakula ndio muhimu na msaada wa kuwezesha kilimo, maji na huduma ya kujisafi, elimu, afya na ulinzi tumezindua katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ombi la dola milioni 331 na habari njema ni kwamba Zimbabwe ina  marafiki na wanaounga mkono na katika wiki mbili tumepokea ahadi kutoka kwa uingeraza ya dola milioni 60, Marekani dola milioni 45 na muungano wa Ulaya dola milioni 11 lakini mahitaji ni mengi na pengo bado ni kubwa.”  

Bwana Parajuli amesema wamelazimika kurekebisha mara tatu ombi la ufadhili kufuatia majanga yaliyoikumba na hali ya uhakika wa chakula huku watu milioni 5.5 wakihitaji msaada na wengine 3.7 walioko hatarni wakihitaji msaada nyongeza juu ya msaada wanaopokea kutoka kwa serikali.

Mratibu Mkaazi huyo amesema hali mashinani inasikitisha hususan pale wenyeji wanakiri kwamba hawawezi kulisha watoto wao wakati huu ambapo mavuno ya mahindi na nafaka zingine ni takriban tani 1.7 inayotaraijwa kila mwaka imeshuka kwa tani laki tisa hivyo kuathiri uhakika wa chakula. Isitoshe harakati za serikali kuimarsiha uchumi na kuzingatia mapato zimeathiri sana hali.

Licha ya changamoto hizo lakini bwana Parajuli amesema kutoa msaada sio suluhu ila

(Sauti ya Parajuli)

“Umoja wa Mataifa na wafadhili wa maendeleo na hata serikali wanatambua hilo na nadhani ndio maana wnataka kubadilisha uchumi na kuleta suluhu ya kudumu, kumekuwa na kampeni nyinig za kualika wawekezaji na wanataka sana kuzingatia sheria na baadhi ya será ambazo hazikuwa zinavutia wawekezaji zimebadilishwa na katika suala la ardhi wanajaribu kuleta sera kuhusu umiliki wa ardhi.”

Bwana Parajuli amerejelea ombi lake la ufadhili kwa ajili ya Zimbabwe kwa jamii ya kimatiafa huku akitoa shukrani kwa wafadhili waliokwisha toa mchanga wao.