Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msumbiji tuko pamoja nanyi kwa hali na mali:Guterres

Mama akimlisha mwanaye wa umri wa miaka miwili katika shule ya Samora Machel ambako waliletwa baada ya nyumba yao kubomolewa na kufurika maji huko Buzi Msumbiji.
UNICEF
Mama akimlisha mwanaye wa umri wa miaka miwili katika shule ya Samora Machel ambako waliletwa baada ya nyumba yao kubomolewa na kufurika maji huko Buzi Msumbiji.

Msumbiji tuko pamoja nanyi kwa hali na mali:Guterres

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu Antonio Guterres, leo ametuma ujumbe maalumu wa mshikamano kwa waathitirika wa kimbunga IDAI , na serikali ya Msumbiji akiahidi kwamba kwa hali na mali Umoja wa Mataifa uko pamoja nao. 

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjini New York Marekani Guterres amesema athari za kimbunga IDAI hazisemeki kuanzia kwenye miundombinu hata hadi huduma za msingi kama vituo vya afya, shule na kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.  Ameongeza kwamba wakati misaada ya kibinadamu ikiendela kufikishwa kwa wathirika Umoja wa Mataifa uko bega kwa bega na watu na taifa hilo la Kusini mwa Afrika na nchi jirani za Malawi na Zimbabwe zilizoathirika pia na mafuriko ya kimbunga hicho,“Leo nataka kurejea kusisitiza mshikamano wangu na watu na serikali za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe . Timu za dharura za Umoja wa Mataifa  na washirika wetu wako huko tangu mwanzo za janga hili . Na katika mazingira magumu tumekuwa tukifikisha msaada wa dharura wa chakula , madawa , vifaa vya kusafisha maji na malazi kwa jamii ambazo bado zimekwama kwenye mafuriko.tumewafikia watu 100,000 na msaada wa chakula na tunaongeza juhudi za kuwafikiwa wengine wengi. Matukio kama haya yanaongezeka na kuwa mabaya zaidi, na hali itakuwa mbaya zaidi endapo hatutochukua hatua sasa.”

Katibu Mkuu pia ametoa wito wa ufadhili haraka kukidhi mahitaji ya waathirika na amemteua  Bwana Marcoluigi Corsi mratibu wa miasaada ya kibinadamu nchini Msumbiji kuimarisha juhudi za Umoja wa Mataifa kukabiliana na athari za kimbunga hicho.

Wakati mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa yakihaha kukidhi mahitaji ya dharura ya waathirika wa kibunga hicho changamoto kubwa ni fedha na leo shirika la umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limetoa ombi la dola milioni 282 ili kuwasaidia watu milioni 1.7 walioathirika nchini Msumbiji kwa masuala ya muhimu kama uhakika wa chakula na Maisha yao, afya, maji , usafi, elimu na malazi.

Naye  mwakilishi wa shirika la Afya dunaini WHOnchini  Musumbiji  Dkt. Djamila Cabral akizungumza kwa njia ya simu kutoka Beira na vitongoji vyake , amesema karibu vituo vya afya 55 vimesambaratishwa na havina uwezo wa kupokea au kuhudumia wagonjwa na hivyo amesema, "kwa WHO, afya ni kipaumbele kwa  sasa. Hatupaswi kuruhusu watu hawa wakabiliwe  na maafa mara mbili kutokana na mlipuko wa magonjwa  au kwa kukosa uwezo wa kupata huduma muhimu za afya. Wameteseka  vya kutosha.

WHO pamoja na mashirika mengine, likiwemo la misaada ya dharra OCHA na la watoto UNICEF  wamesema wamejiandaa kutoa usaidizi  endapo milipuko ya magonjwa  ya kuhara,  kipindupindu , chanjo  na magonjwa mengine ya dharura kwa zaidi ya watu 900,000 .