WFP yataka fedha zaidi ili kuimarisha mgao wa dharura Zimbabwe

Nchini Zimbabwe ambako wengi wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula.
WFP/Tatenda Macheka
Nchini Zimbabwe ambako wengi wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula.

WFP yataka fedha zaidi ili kuimarisha mgao wa dharura Zimbabwe

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, linaongeza kwa haraka operesheni za dharura nchini Zimbabwe ambako kiangazi, mafuriko na hali ngumu ya uchumi vimesababisha watu milioni 7.7 kujikuta katika hali mbaya ya njaa. 

Mkurugenzi Mkuu wa WFP David Beasley amesema fdola milioni 293 zinahitajika kwa haraka kwa kuwa shirika hilo liweze kutimimzia mahitaji yanayoongezeka ya watu walioathirika vibaya nchini Zimbabwe, lakini hata hivyo hadi sasa ni asilimia 30 tu ya fedha hizo ndio zimepatikana.

Hali ni mbaya akisema kuwa hivi sasa wako kwenye mzunguko wa janga la utapiamlo ambalo linaathiri zaidi wanawake na watoto na kwamba kwa sasa itakuwa vigumu sana kuondokana na tatizo hilo.

Kwa mantiki hiyo amesema fedha hizo zitasaidia mpango wa WFP wa kuongeza maradufu idadi ya wale inaowasaidia ifikapo mwezi ujao wa Januari hadi watu milioni 4.1 ikitoa migao ya nafaka, mafuta ya kupikia na lishe nyingine kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

Janga la njaa nchini Zimbawe, lililo baya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya miaka 10 , ni sehemu moja ya hali iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi yanaoshuhudiwa sasa Kusini mwa Afrika.

Viwango vya joto eneo hilo vinaongezeka kwa zaidi ya mara mbili ya vile vya dunia na misimu ya mvua isiyotarajiwa inawaathiri vibaya wakulima.

Janga hilo linachochewa zaidi na uhaba ya fedha za kigeni, mfumuko wa uchumi,kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, uhaba wa mafuta, kupotea kwa kawi kwa muda mrefu na kufa kwa mifugo wengi, hali inayowaathiria wakaaji na mijini na pia vijini kwa viwango sawa.