UN yaongeza juhudi za msaada kwa Morocco na Libya kutokana na maafa yaliyowasibu: Griffiths
Zahma kubwa mbili tofauti kabisa nchini Morocco na Libya zikiunganishwa na maumivu makubwa ya familia zilizofiwa, zinaendelea kuhamasisha juhudi za Umoja wa Mataifa za kutoa misaada,amesema leo afisa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Martin Griffiths.