Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaunda kamati kuchunguza matukio ya Idlib Syria

Msichana wa umri wa miaka saba asimama mbele ya jengo la shule lililoharibiwa  mjini Idlib Syria.
UNICEF
Msichana wa umri wa miaka saba asimama mbele ya jengo la shule lililoharibiwa mjini Idlib Syria.

UN yaunda kamati kuchunguza matukio ya Idlib Syria

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameamua kuunda kamati ya uchunguzi ili kutathimini mfululizo wa matukio yaliyofanyika Kaskazini Magharibi mwa Syria tangu kutiwa saini makubaliano ya kurejesha utuli wa hali ya taifa hilo la Mashariki ya Kati kwenye eneo la Idlib baina ya Urusi na Uturuki mnamo 17 Septemba 2018.

Kupitia tarifa iliyotolewa leo na msemaji wake Guterres amesema “Uchunguzi utajikita katika uharibufu au madhara katika majengo yaliyo kwenye eneo lisilitakiwa kuwa na mapigano na majengo yanayosaidiwa na Umoja wa Mataifa katika kanda hiyo.”

Na kamati ya ndani ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa itatathimini na kuhakiki ukweli wa matukio hayo na kutoa ripoti kwa katibu Mkuu tathimini yao ikikamilika.

Katibu mkuu amezitaka pande zote husika kushirikiana na kamati hiyo pindi itakapoanza kazi rasmi.

Jumanne wiki hii mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock aliwashutumu wajumbe wa Baraza la Usalama kwa kutochukua hatua dhidi ya "mauaji" yanayoendelea huko Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.

"Kwa zaidi ya siku 90, uvurumishaji wa makombora uliofanywa na serikali ya Syria, inayoungwa mkono na Shirikisho la Urusi, umesababisha mauaji katika eneo lisilotakiwa mapigano la Idlib” amesema Lowcock. Mauaji na kutokujali kwa jamii ya kimataifa ambako tayari kulikuwa kumeshutumiwa na mkuu wa haki za binadamu waUmoja wa Mataifa  Michelle Bachelet Ijumaa iliyopita.