Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nini maana ya nyumbani? na kwa wakimbizi nyumbani ni wapi: mshairi Bigoa Chuol

Kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini akiwa amefika ukimbizini Uganda.
UNICEF/UN068615/Oatway
Kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini akiwa amefika ukimbizini Uganda.

Nini maana ya nyumbani? na kwa wakimbizi nyumbani ni wapi: mshairi Bigoa Chuol

Wahamiaji na Wakimbizi

Baada ya kuishi ukimbizi kwa zaidi ya miongo miwili mshairi Bigoa Chuol kutoka Sudan kusini ameamua kutumia kipaji chale kuhoji “nini maana ya nyumbani? na kwa wakimbizi nyumbani ni wapi? 

Bigoa Chuol ni mshairi na mkimbizi akisema yeye ni Msudan Kusini wa kurith,  kwa zaidi ya miongo miwili amekuwa akisafiri huku na kule na kisha kuishi ukimbizi na kupitia talanta yake ya ushairi anahoji maana halisi ya ‘nyumbani” hususan kwa wakimbizi kama yeye. Shairi lake “Birth water” ni kionjo tu cha mgogoro unaoghubika fikra zake kati ya asili yake alikozaliwa na anakoishi sasa akijihisi ndiko nyumbani na ni sehemu ya jamii yake.

(BIGOA -SHAIRI)

“Linaitwa maji ya kuzaliwa ni kutaka kubaini uzoefu wa kuwa Msudan Kusini, na  hii ina maana gani, na kwa yale niliyopitia kama mkimbizi na pengine katika umri mdogo na bila kuelewa na ha bila kuelezewa hadithi hiyo. Ninapoifikiria hili ni kama unaingia tena katika sakata jipya, katika vita vipya ambavyo ni mtihani mkubwa kabisa”

Bigoa Chuol mwenye umri wa miaka 28 yeye na familia yake walikimbia vita Sudan Kusini akiwa mtoto na amesikia hadithi ya jinsi mama yake alivyombeba kichwani akiwa ndani ya ndoo hadi nchi jirani ya Ethiopia ili kunusuru maisha yake, kisha wakakimbilia Kenya. Na alipotimiza miaka 11 kwa masaada wa mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, yeye na familia yake walipelekwa nchi ya tatu, Australia na kupata makazi ya kudumu hadi sasa ni miaka 17. Kama mkimbizi bado kwake fikra za wapi ni nyumbani imekuwa kitendawili

(SAUTI YA BIGOA CHUOL)

“Ukiwa umepitia madhila ya kufurushwa na vita na kutokuwa na hisia za usalama na utulivu, huwezi. Huwezi haraka kubaini mizizi ya chimbuko lako. Kwa hiyo, sijawahi kujihisi kama nimeondoka mahali kwa sababu sidhani kama nimekuwa nikipahisi ni nyumbani. "

Vita vya Sudan Kusini viewalazimisha watu milioni 4 kukimbilia nchi jirani na wengine kuwa wakimbizi wa ndani, waathirika wakubwa wakiwa ni watoto na wanawake. Sasa Bigoa anatumai kusambaza ujumbe wa athari za vita kwa kila mkimbizi kupitia ushairi.