Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 8 ya uhuru Sudan Kusini imeghubikwa na machafuko sasa imetosha:UNHCR

Watoto wawili walioachliwa na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini wanasimama katika shereheya kuwaachilia mjini Yambio kabla ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia.
UNICEF/Sebastian Rich
Watoto wawili walioachliwa na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini wanasimama katika shereheya kuwaachilia mjini Yambio kabla ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia.

Miaka 8 ya uhuru Sudan Kusini imeghubikwa na machafuko sasa imetosha:UNHCR

Amani na Usalama

Shiri la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeisihi serikali ya Sudan kusini, wapinzani na wananchi kuhakikisha wanaongeza juhudi za kupatikana amani ya kudumu na kuwaondolea mamilioni ya watu wan chi hiyo adha kubwa wakati huu ikiadhimisha miaka 8 ya uhuru.

Ikiwa leo ni miaka 8 kamili tangu taifa hilo changa kabisa kujinyakulia uhuru wake limekuwa likighubikwa na vita, machafuko na madhila kwa wananchi ambao maelfu wamelazimika kukkfungasha virago kwenda kusaka usalama. Lakini sasa UNHCR inasema kufuatia makubaliano ya amani yaliyotoiwa saini 12 Septemba 2018 kuna matumaini kwani yameweka msingi kwa ajili ya amani , hatua zimepigwa ingawa bado kuna changamoto na amani inaonekana kuwa ni tunda la mbali mtini. Akifafanua kuhusu hilo msemaji wa UNHCER mjini Geneva Uswis Charlie Yaxley amesema “UNHCR inaamini kwamba ni muhimu kwa wawakilishi kutoka jamii za wakimbizi na wakimbizi wa ndani, kushiriki  kikamilifu katika mchakato wa amani. Mkataba wowote wenye ushawishi ni lazima ujumuishe mawazo bayana nay a wazi kwa ajili ya upatanisho. Mbinu za kupata haki lazima ziwe wazi na za kuaminika. Wasudan Kusini wengingi wametawanya Zaidi ya mara moja, na Imani yao katika mchakato huu ni muhimu sana ili ufanikiwe.”

Ameongeza kuwa mawazo pia ni lazima yaweke kipaumbele kwa vijana kwani machafuko yanayoendelea yameathiri kwa kiasi kikubwa watoto ambao ni takribani theluthi mbili ya wakimbizi wote nchini Sudan Kusni. Shirika hilo la wakimbizi limesisitiza kuwa ili Sudan Kusini iweze kuwa taifa la amani na mafanikio ni lazima kuwahakikishia vijana wan chi hiyo wakiwemo wakimbizi fursa ya elimu bora na zingine za kutimiza ndoto zao.

Zaidi ya raia milioni 2.3 wa Sudan Kusini hivi sasa wanaishi kama wakimbizi katika nchi jirani , huku wengine milioni 1.9 ni wakimbizi wa ndani katika taifa hilo.

Sasa UNHCR na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wametoa ombi la dola bilioni 1.4 ili kuweza kutoa misaada muhimu ya kibinadamu kwa wakimbizi . Hadi sasa ni asilimia 21 tu ya ombi hilo ndio iliyofadhiliwa na shirika hilo linasema mahitaji ya wakimbizi yamezidi uwezo wa fedha zilizopo.