Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea yatoa tani 5,000 za chakula kwa wakimbizi, Uganda

Wakuu wa wakimbizi na mwakilishi wa UNHCR wakipokea mgao wa mchele kutoka Korea, Nakivale, Uganda.
WFP/Lydia Wamala
Wakuu wa wakimbizi na mwakilishi wa UNHCR wakipokea mgao wa mchele kutoka Korea, Nakivale, Uganda.

Korea yatoa tani 5,000 za chakula kwa wakimbizi, Uganda

Wahamiaji na Wakimbizi

Shrika la Mpango wa chakula duniani (WFP) nchini Uganda limekaribisha mchango tani 5,000 za mchele kutoka kwa seriakli ya Korea Kusini amabyo imeitikia mahitaji ya cahkula yanayongezeka kila uchao miongoni mwa wakimbizi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa (WFP) limepokea mchango huo hii leo na kusema kwamba umekuja wakati amabpo ulikuw aunahitajika mno ikizingatia ongezeko la idadi ya wakimbizi kutoka nchi jirani hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

 Kwenye sherehe ya kukabidhi mchango huo iliyofanyika katika kambi ya wakimbizi ya Nakivale wilayanai Isingiro, El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa WFP, Uganda amesema msaada huo utasaidia kushughulikia mahitaji ya chakula kwa wakimbizi Zaidi ya 200,000.

 Amesema wengi wa wanufaika watakuwa ni wale wanaotorka mizozo ya bunduki na njaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ili waweze kuanza maisha mapya ukimbizini.

 Dholoum ameongeza kuwa mchele huo utaimarisha lishe kwa wakimbizi ambao mnamo Julai na Agosti walikuwa wapokee unga wa mahindi kama mgao wao wa kila mwezi, katika kambi za wakimbizi za Kyaka II, Kyangwali, Nakivale, Oruchinga na Rwamwanja.

 Ha Byung-Kyoo, Balozi wa Korea Kusini nchini Uganda amesema wametoa msaada huo kwani serikali na watu wa Koread Kusini wameguswa na maisha magumu wanaopitia wanawake na watoto ambao wanakimbia mgogoro nchini mwao.

 Pia mwaka jana Korea Kusini itoa tani 5,000 za mchele kwa ajili ya kulisha wakimbizi Uganda.