Twahitaji dola milioni 927 kukidhi mahitaji ya wakimbizi:Uganda/ UNHCR

28 Mei 2019

Serikali ya Uganda kupitia ofisi ya waziri mkuu OPM, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wengine wanaosaidiana nao katika kukabiliana na wimbi kubwa kabisa la wakimbizi Afrika Mashariki , leo wamezindua ombi kwa wahisani la dola milioni 927 ili kushughulikia mahitaji ya wakimbizi Zaidi ya milioni 1.3 wanaotarajiwa nchini Uganda ifikapo mwisho wa 2020.

UNHCR inasema fedha za ombi hilo pia zitatumika kuzisaidia jamii za wenjyeji katika wilaya zinazohifadhi wakimbizi. Machafuko na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRCna mivutano yenye mrengo wa kikabila inayoendelea nchini Sudan Kusini vimewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia na kwenda kusaka hifadhi nje ikiwemo Uganda ambako mamia huingia kila siku.

Zaidi ya maishirika 100 ya kitaifa na kimataifa yamiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na UNHCR na OPM katika makakati wa sasa wa kuwasaidia wakimbizi nchini Uganda ujulikanao kama RRP.

 Msaada unaotolewa

 Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akisalimiana na watoto wakimbizi wakati wa ziara yake huko kambi ya wakimbizi ya Imvepi nchini Uganda
UN
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akisalimiana na watoto wakimbizi wakati wa ziara yake huko kambi ya wakimbizi ya Imvepi nchini Uganda

Mkakati huo wa msaada kwa wakimbizi unajumuisha mchakato wa kuhakikisha huduma za msingi zinapatikana kwa wakimbizi hao kama maji safi na salama , masuala ya usafi, huduma za afya na lishe, chakula, malazi, elimu, ulinzi wa kimazingira , msaada wa maisha na huduma za ulinzi.

Na kwa mujibu wa wadau wa RRP kipaumbele ni ulinzi na huduma za dharura , kuongeza fursa za elimu , kujeresha mazingira salama na msaada wa kujikimu kimaisha. Wanasema viapumbele hivi na hususan  elimu na maziringa ni muhimu sana katika kuhakikisha jamii zinazowahifadhi haziathiriki vibaya , katika kuhakikisha kunakuwepo na amani katika kuishi pamoja miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi lakini pia kudumisha ukarimu wa Uganda kwa wakimbizi hao.

Mpango wa RRP unajumuisha pia mikakati ya kuongeza uwezo wa wa watoa huduma wa kijamii zikiwemo mamlaka za wilaya.

Takribani robo ya wanaopokea huduma za elimu na afya ziliazoanzishwa kupitia mkakati wa wakimbizi ni wenyeji raia wa Uganda. Mkakati huo ulifanyiwa marewkebisho kidogo katika bajeti yake ya jumla na kupunguzwa kidogo kufuatia tathimini ya idadi kamili ya wakimbizi waliorodheshwa nchini Uganda mwaka 2018.

Idadi ya wakimbizi Uganda

Idadi kamili ya wakimbizi walioko Uganda hivi sasa inajumuisha wakimbizi wapya walioongezeka tangu 2018, na kuifanya nchi hiyo sasa kuhifadhi wjumla ya wakimbizi milioni 1.25 huku idadi hiyo itarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 1.3 mwishoni mwa mwaka 2020, ikizingatiwa kwamba kunaweza kuwa na mazingira tofauti yanatakayozuia wimbi la wakimbizi kuingia, kudhibitiwa kwa ongezeko la idadi ya watumazingira tofauti na wakimbizi wengine kujerea nyumbani kwa hiyari.

Ombo la leo limekuja wakati wadau wa RRP wanashuhudia changamoto kubwa ya ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji ya wakimbizi nchini Uganda. Kwa mujibu wa waziri wa maandalizi na udhibiti wa majanga na wakimbizi nchini Uganda Injinia Hilary Onek “ Uganda inahitaji haraka msaada wa kifedha na mshikamano kutoka kwa washirika ili kutuwezesha kukabiliana na ongezeko la idadi ya wakimbizi na ili tuweze kuwapokea, kuwaandikisha na kuwatengea ardhi na makazi, huku wakati huohuo tukizisaidia jamii zinazowahifadhi.”

Wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwasili kwenye kituo cha  muda cha mapokezi huko Sebagoro, wilaya ya Hoima nchini Uganda
UNHCR/Michele Sibiloni
Wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwasili kwenye kituo cha muda cha mapokezi huko Sebagoro, wilaya ya Hoima nchini Uganda

Changamoto zilizopo

Hivi sasa UNHCR na wadau wa RRP wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kudumisha huduma zilizopo katika makazi ya wakimbizi, kutimiza viwango vya chini vya utoaji huduma za msingi , kuendesha na kuendeleza huduma za maji, afya namiundombinu ya elimu ikiwemo barabara zinazofanya kazi na kupitika na masuala mengine ya kiufundi.

Na uwezo wa kuwekeza kwa wakati muafaka na kwa muda mrefu na pia huduma endelevu vimeathirika vibaya kutokana na ukata.

Mwaka 2018 asilimia 57 tu ya bajeti ya RRP ndio iliyofadhiliwa na kuacha mahitaji mengine mengi ya lazima kutotimizwa. Michango yam waka 2019 imekuwa ikija polepole sana na mpaka sasa ni chini ya asoilimia 20 ya fecha zinazohitajika ndio zimepatikana .

Endapo kiwango cha misaada kitaendelea kusuasua kama sasa bila kuongezeka basi athari zake zitakuwa mbaya , Watoto wengi Zaidi hawatosoma kutokana na kukatwa kwa fungu la elimu, kukosa uwezo wa kuzuia magonjwa ya mlipuko ikiwemo ebola, hali ya usafi kuwa mbaya, kupunguza hatua za kupambana na ukatili wa kingono na wa kijinsia (SGBV), kuongeza mzigo wa madhila kwa wanawake na Watoto ambao ni asilimia 83 ya wakimbizi wote.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter