Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wale wanaokimbia Venezuela wanahitaji kupewa ulinzi wa kimataifa - UNHCR

Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini  Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.
© UNHCR/Stephen Ferry
Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.

Wale wanaokimbia Venezuela wanahitaji kupewa ulinzi wa kimataifa - UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutokana na hali ya kisiasa, kiuchumi na ya haki za binadamu kuzidi kuzorota nchini Venezuela ambayo saa imewalazimu watu milioni 3.7 kuondoka,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuwa wengi wa wale wanaokimbia nchi wanastahili kupewa usalama  na ulinziwa kimataifa.

Ripoti iliyotolewa leo, na UNHCR imerejelea wito wake ikizitaka nchi kuruhusu raia wa Venezuela kuingia na kuwapa ulinzi unaostahuili na huduma zingine. Hadi mwisho wa mwaka 2018, takriban watu 460,000 raia wa Venezuela walitafuta hifadhi, wengie kweye nchi majirani za Amerika ya Kusini.

Ripoti hiyo inasema kuwa asilima kubwa ya raia wa Venezuela wanahitaji kupewa ulinzi wa kimataifa kwamujibu wa mkataba wa mwaka 1984 uliotekelezwa Amerika ya Kusini. Hii ni kutoka na vitisho vilivyoko dhidi ya maisha yao kufuatia hali ilivyo  sasa nchini Venezuela.

Kwa pamoja na mshirika wetu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), tumekaribisha kila mara uzalendo wa serikali za Kusini mwa Marekani na zile za Caribbean lwa kuwapa makaoa raia wa Vezuela, imesema ripoti ya UNHCR.

UNHCR pia iliziomba nchi kuhakisha kuwa raia wa Vezualha licha ya hali waliyo nayo wasirudishwe makwao kwa lazima.

UNHCR inasema inashikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji na serikali na pia mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kushughulikia mahitaji ya usalama ya wakimbizi wa Venezuela na na pia wahamiaji.