Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa jamii ya watu wa asili wameimarisha stadi kwa msaada wa Illaramatak Kenya

Wanawake kutoka kabila la wasamburu nchini Kenya
UNICEF/Samuel Leadismo
Wanawake kutoka kabila la wasamburu nchini Kenya

Wanawake wa jamii ya watu wa asili wameimarisha stadi kwa msaada wa Illaramatak Kenya

Utamaduni na Elimu

Shirika la Illaramatak Community Concerns nchini Kenya ambalo linahusika na kusaidia jamii za wafugaji limesema kuwa baada ya harakati za kuhamasisha jamii na hususan wanawake kuzaa matunda sasa limejikita katika kuwawezesha wanawake kwa ajili ya kusaidia kusongesha mbele jamii kwa ujumla. 

Agnes Leina ambaye ni mwanzilishi wa shirika lisililo la kiserikali la Illaramatak Community Concerns amesema hayo akihojiwa nami mapema mwaka huu kwenye Umoja wa Mataifa, Bi Leina amesema kufuatia ufadhili aliopokea alianzisha kituo cha wanawake ambapo

“Baada ya kuwahamasisha nimechukua hatua ya pili ambapo kufuatia ufadhili tumefungua kituo ambacho wanawake wanashona sare za shule kwa ajili ya wanafunzi huku zingine tukiwapa watoto wasio jiweza au waliokimbiz changamoto mbali mbali, mradi ambao tumeupa jina cut the garment not tha girl yaani kata kitambaa sio msichana.”

Kwa kawaida wanawake wa jamii ya asili wanafahamika kwa kazi zao za shanga lakini katika juhudi za kuwawezesha wamepokea pia stadi zingine kama anavyoelezea Bi. Leina.

“Kwa kawaida wanawake wa jamii ya asili wana ujuzi wa kutengeneza shanga laini sasa nimewaleta vijana ambao wametoa mafunzo ya kushona zulia na kadhalika.”

 

TAGS: Jamii ya watu wa asili, Maasai, Samburu, Kenya, wanawake