wanwake

Virusi vya Corona vyasababisha kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa CSW

Virusi vya Corona au COVID-19 vimeendelea kuathiri shughuli a kiuchumi, kijamii na kisiasa duniani na athari hasi za hivi karibuni zaidi ni kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliokuwa ufanyike kwa wiki mbili hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 9 hadi 20 mwezi huu wa Machi.

Wanawake wa jamii ya watu wa asili wameimarisha stadi kwa msaada wa Illaramatak Kenya

Shirika la Illaramatak Community Concerns nchini Kenya ambalo linahusika na kusaidia jamii za wafugaji limesema kuwa baada ya harakati za kuhamasisha jamii na hususan wanawake kuzaa matunda sasa limejikita katika kuwawezesha wanawake kwa ajili ya kusaidia kusongesha mbele jamii kwa ujumla. 

Tunachokipigania Tanzania sio idadi tu bali pia ubora wa wanawake viongozi: Ummy Mwalimu

Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika harakati za ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali iikiwemo kijamii, kiuchumi na hata kisiasa. Flora Nducha na tarifa zaidi

Wanawake wa Zanzibar ya leo, sio kama wale tulioyowazoea, wakiletewa kila kitu na waume zao.

Serikali ya Zanzibar imepiga hatua muhimu  katika masuala ya ukombozi wa mwanamke kama ilivyo katika ya ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 , kuhakikisha mwanamke huyo anapata usawa kwa kijinsia, kiuchumi na kijamii.

Mazingira yaweza kuwakomboa wanawake -Grassroot Women Initiative Network

Wanawake katika sehemu mbali mbali duniani wanajikita katika mbinu tofauti kwa ajili ya kubadilisha maisha yao na ya jamii wanakoishi na kwingineko hususani mazingira yanayowazunguka.

Sauti -
3'55"

Zaidi ya kuwa mhandisi, Nadhifa Zubeir ni mama na mke

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, katika masomo ya ngazi ya juu takribani asilimia 30 pekee ya wanafunzi wa kike ndiyo wanachagua masomo yanayohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.

Sauti -
3'19"

Mwalimu wa kike aanzisha biashara inayotoa fursa za ajira kwa wengine Uganda

Wanawake wanajumuisha takriban asilimia 52.5 ya nguvu kazi na ni kiungo muhimu katika kufanikisha melengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan katika sekta ya ujasiriamali kwenye biashara ndogo ndogo na za wastani.

Sauti -
3'59"