Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa Zanzibar ya leo, sio kama wale tulioyowazoea, wakiletewa kila kitu na waume zao.

Wanawake wajasiriamali kama huyu wakipatiwa mafunzo ya biashara watakwamua sio tu familia zao bali pia jamii zao
ILO/screen capture
Wanawake wajasiriamali kama huyu wakipatiwa mafunzo ya biashara watakwamua sio tu familia zao bali pia jamii zao

Wanawake wa Zanzibar ya leo, sio kama wale tulioyowazoea, wakiletewa kila kitu na waume zao.

Ukuaji wa Kiuchumi

Serikali ya Zanzibar imepiga hatua muhimu  katika masuala ya ukombozi wa mwanamke kama ilivyo katika ya ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 , kuhakikisha mwanamke huyo anapata usawa kwa kijinsia, kiuchumi na kijamii.

Hilo limedhihirishwa na miradi mbalimbali iliyoanzishwa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambako kwa miaka mingi mwanamke alionekana kuwa tegemezi na kama pambo la nyumbani. Moja kati ya miradi iliyoanzishwa ni pamoja na Barefoot College,  chuo kinachotoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa wanawake wa vijijini huko visiwani ikiwa ni pamoja na elimu ya kutengezeza paneli za nishati ya jua au sola.

Pendo Daudi ni mratibu wa chuo hicho cha  Barefoot anafafanua lengo la mradi huo, "Barefoot inajihusisha na masuala ya uwezeshaji kwa wanawake. Tunawawezesha wanawake,t unafundisha kuwa ma sola injiniaz au tunapenda kuwaita sola mamaz. Wanajifundisha jinsi ya kufunga zile sola jinsi ya kusifanyia kazi, na jinsi ya kuzitengeneza zinapokuwa zimeharibika"

Na kuhusu vigezo vilivyowekwa kuwasajili wanafunzi wa chuo hicho Pendo anasema,"tunachokifanya tunaenda kijijini ,tukifika kijijini tunakaa na jamii nzima ya pale kijijini. Viongozi wa kidini viongozi wa serikali, wazee, wamama wababa, wote tunakaa nao pamoja . Kwa Pamoja tunwambia kuwa tunahitaji mwanamke ambaye anaweza kuja chuoni akasoma ili aweze kurudi akawafungia umeme. Kwahiyo sisi tunasifa za mwanamke ambaye tunamtaka. Awe hajasoma awe na umri kwanzia miaka 35 mpaka 55, asiwe na mtoto chini ya miaka 5, asiwe na undugu na kiongozi yeyote wa serikali kwasababu hatutaki upendeleo. Tunaka huu mradi umguse yule ambaye hana tegemezi kabisa katika kile kijiiji au nchi husika. Sisi hatuwafahamu hao wanawanke lakini wanakijiji wanawafahamu."