Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya watu wote CAR hawana uhakika wa chakula:WFP

Takribani tani 160 za chakula kutoka Uganda zilipelekwa huko Zemio nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kupitia Uganda ili kusaidia wakimbizi wa ndani.
UN /Herve Serefio
Takribani tani 160 za chakula kutoka Uganda zilipelekwa huko Zemio nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kupitia Uganda ili kusaidia wakimbizi wa ndani.

Zaidi ya nusu ya watu wote CAR hawana uhakika wa chakula:WFP

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Takriban nusu ya watu wote nchini Jamhuri ya Africa ya Kati au CAR, ambao ni sawa na watu zaidi ya milioni 1.8 wanakabiliwa na zahma kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula.

Kwa mujibu waripoti mpya ya kiwango cha hali ya uhakika wa chakula (IPC) ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, iliyotolewa leo vita, kutokuwepo na usalama, watu kutawanywa na gharama za juu za bei ya vyakula vinalitumbukiza taifa hilo katika janga kubwa la njaa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa WFP Herve Verhoose amesema

SAUTI HARVE VERHOOSE

Zaidi ya watu milioni 1.8 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula na hawajuo wapi utakakakotola mlo wao unaofuata wakati wa msimu wa muambo  ulioanza Mei hadi Agosti.

Ripoti hiyo iliyokubaliwa na jumuiya ya kimataifa inatoa mgawanyoa wa kiwango cha upungufu wa chakula katika ngazi 5, ambapo ngazi ya 1 ni tatizo dogo na ngazi ya tano ni janga kubwa nan chi CAR watu milioni 1.8 wako katika ngazi ya 3 ambayo ni mgogoro mkubwa huku wengine Zaidi ya 465,000wako katika hali ya dharura katika msimu huu wa muambo ambayo ni ngazi 4.

Ripoti imeongeza kuwa waathirika Zaidi ni watu kwenye maeneo yenye kundi kubwa la waliotawanywa la Bria, Kaga- Bandoro, Obo, Rafai na Zemio, na hali ya dharura ipo katika maeneo ya Mbomou, Haute, Kotto na Haut Mbomou. Akifafanua Zaidi kuhusu hali hii Verhoose amesema

SAUTI YA HARVEY VERHOOSE

Karibu watu milioni 1.35 takriban asilimia 30 ya watu wote waliofanyiwa tathimini watakuwa katika hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula wakiwemo karibu watu 274,000 ambao watakuwa katika hali ya dharura wakati wa msimu mavuno katika kipindi cha kati ya Septemba na Oktoba 2019.

Pia inakadiriwa kwamba maeneo matatu yenye idadi kuwa ya watu waliotawanywa na machafuko yatasalia katika hali ya dharura ya uhakika wa chakula. Maeneo hayo kwa ujumla yanawatu 620,000 na licha ya makubaliano yaliyotiwa saini Bangui Februari mwaka huu hali ya usalama bado ni mbaya katika majimbo hayo.