Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na WFP waadhimisha siku ya chakula duniani nchini Libya

Mpishi Ron Pickarski akikatakata mboga jikoni kwake Boulder Colorado
©FAO/Benjamin Rasmussen
Mpishi Ron Pickarski akikatakata mboga jikoni kwake Boulder Colorado

FAO na WFP waadhimisha siku ya chakula duniani nchini Libya

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo dduniani FAO na la mpango wa chakula WFP wameadhimisha siku ya chakula dunini nchini Libya kwa miradi maalumu ya kuisaidia nchi hiyo kufikia lengo la maendeleo la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa WFP nchini Libya Saber Abdeljaber wanafanyakazi na FAO na jamii kwa kushirikiana na serikali ya Libya ili katika miaradi hiyo ili kuimarisha uhakika wa chakula na kujenga mnepo. Ameongeza kuwa “Kwa upande wa WFP moja ya mradi ambayo ni muhimu sana kwetu ni mradi wa mlo shuleni ambao tumeuzindua kwa ushirikiano na wiraza ya elimu ya serikali ya Libya.”

Mwezi septemba mwaka huu WFP na wizara ya elimu ya Libya walizindua programu ya lishe ya majira ya joto na kuwagawia watoto chakula programu ambayo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuhudhuriwa na watoto 600 nchini nzima.

Lengo la programu hiyo ilikuwa ni kuelimisha watoto na wazazi wao kuhusu umuhimu wa lishe bora na mazoezi kwa ajili ya afya kuwa ni sehemu ya mradi wa mlo mashuleni ambao unalenga kuwafikia watoto 20,000 mwaka huu na kupanua wigo hadi kuwafikia watoto 40,000 nchini nzima kuanzia Januari mwakani.

FAO imeelezea umuhimu wa ushirikiano wao na WFP na mashirika mengine ya misaada na pia wizara ya kilimo ya Libya, vizara ya mifugo, maji na rasilimali za baharí pamoja na vyuo vikuu katika kufanikisha ajenda ya kuwasaidia mamilioni ya watu wanaohitaji msaada.

Wakati tunafanya kila tuwezalo kuelekea utokomezaji wa njaa , FAO inaamini katika kuwekeza katika mustakabali bora katika chakula na kilimo kwa kushirikiana na wadau wengine “ amesema mwakilishi wa FAO Libya Mohhamed Al-Ansi na kuongeza kuwa “Siku ya chakula duniani ni kumbusho zuri wakati FAO ikisherehekea miaka 74 tunawaalisha wote kushiriki katika siku ya chakula duniani shindano la picha ambalo litaendelea hadi Novemba 8.”

Libya imeghubikwa na vita ambayo vimevuruga utulivu w anchi hiyo , usalama, uchumi na hali ya kibinadamu katika miaka minane iliyopita. Uhakika wa chakula umeendelea kuwa changamoto kutokana na mamilioni ya watu kutawanywa, kuingilia biashara na kuzorota kwa uzalishaji wa chakula .

Hata hivyo licha ya changamoto zote hizo serikali ya Libya na watu wake wanajitahidi kufanya kila wawezalo kurejesha utulivu na amani nchini mwao. WFP na FAO wamejizatiti kusaidia ujenzi wa Libya imara kupitia mikakati nanushirika kama ule walionao na wizara ya elimu na wizara ya kilimo.