Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kutambua, na kushikamana na watu wenye ualibino:UN

Ualibino na hali ambayo ni nadra , ya kurithi na mtu huzaliwa nayo. Inawapata wato wote wa jinsia ya kiume na ya kike bila kujali asili na ni katika nchi zote duniani
Corbis Images/Patricia Willocq
Ualibino na hali ambayo ni nadra , ya kurithi na mtu huzaliwa nayo. Inawapata wato wote wa jinsia ya kiume na ya kike bila kujali asili na ni katika nchi zote duniani

Ni muhimu kutambua, na kushikamana na watu wenye ualibino:UN

Haki za binadamu

Siku ya kimataifa ya uelewa kuhusu watu wenye ualibino ni wakati wa “kutambua, kusherehekea na kushikamana na wayu wenye ualibino kote duniani” umesema Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku hiyo inayosherehekewa kila mwaka safari hii ikibeba kauli mbiu “bado tunasimama imara.

Kila mwaka Juni 13 dunia inakumbushwa kwamba watu wenye ualibino wanastahili kuwa na haki yao ya kuishi na kulindwa. Mara nyingi watu hawa hukabiliwa na changamoto nyingi dhidi ya haki zao za binadamu kuanzia unyanyapaa naubaguzi , hadi vikwazo katika masuala ya afya na elimu.

Ualibino ni hali ambayo ni ya nadra na ya kurithi ambayo mtu huzaliwa nayo. Hali hii haiambukizi na inawapata wote wanawake na wanaume bila kujali kabila au asili yao katika nchi zote duniani.

Changamoto za kiafya

Kukosa madini yanayotengeneza rangi au melanin katika nywele, Ngozi na macho vinamuweka mtu katika hatari dhidi ya jua na mwanga mkali na matra nyingi huwasababibishia watu wenye ualibino kupoteza ngumu ya macho kuuona au upofu na hatari ya kupata saratani ya ngozi.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa katika baadhi ya nchi asilimia kubwa ya watu wenye ualibino hufariki dunia kutokana na saratani ya ngozi katika umri wa kati ya miaka 30 na 40. Ingawa inaweza kuzuilika endapo haki zao za kiafya zitatekelezwa hatua hizo ni pamoja na upatikanaji wa mafuta maalum ya Ngozi yanatakayowakinga na jua, kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu wa mara kwa mara , kupata nguo zitakazowakinga na mionzi mikali ya jua  na miwani maalum vifaa ambavyo mara nyingi hawavipati au havipatikani katika nchi nyingi.

Watoto marafiki wakitembea kurudi nyumbani baada ya muda wa shule huko nchini Ivory Coast. Watu wenye ualbino wamekuwa wakikabiliwa na unyanyapaa na ukatili katika baadhi ya nchi kama ilivyo Malawi.
UNICEF/Frank Dejongh
Watoto marafiki wakitembea kurudi nyumbani baada ya muda wa shule huko nchini Ivory Coast. Watu wenye ualbino wamekuwa wakikabiliwa na unyanyapaa na ukatili katika baadhi ya nchi kama ilivyo Malawi.

Kutokana na ukosefu wa madini ya melanin watu wenye ualibino siku zote huwa na matatizo ya macho ambayo mara nyingi huwasababishia ulemavu wa kutoona na katika masuala ya ,maendeleo wao huwa ni miongoni mwa makundi yanayosalia nyuma, hivyo Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba watu wenye ualibino wanahitaji kupiganiwa haki zao za binadamu kwa misngi ya kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s.

Ubaguzi

Watu wenye ualibino pia hukabiliwa na ubaguzi mkubwa kutokana na rangi ya Ngozi yao lakini pia kwa sababu ya ulemavu na Zaidi ya hayo hawaonekani au kutambulika mara nyingi katika njyanza za kijamii au majukwaa ya kisiasa. Wakati idadi inatofautiana inakadiriwa kwamba Amerika ya Kaskazini na Ulaya mtu mmoja kati ya 17,000 au 20,000 ana ualibino. Hali ni tofauti Afrika Kusini mwa jangwa la sahara kukikadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya 1400 ana ualibino nchini Tanzania huku Zimbawe idadi ikiwa mtu 1 kati ya 1000 na katika makundi mengine Kusini mwa Afrika kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Na ubaguzi dhidi ya watu hawa hutofautiana pia wakati Amerika ya Kaskazini, Ulaya na Australia mara nyingi ni kudhihakiwa, kuitwa majina, kutaniwa na kuonewa wakiwa wadogo.

Kuna taarifa chache kuhusu maeneo mengine kama Asia, Amerika Kusini na Pasifiki. Hata hivyo Umoja wa Mataifa umeainisha kwamba kwa mujibu wa ripoti nchini China nan chi zingine za Asia Watoto wenye ualibino wanakabiliwa na hali ya kutelekezwa na kukataliwa na familia zao.

Barani Afrika takwimu zinaonyesha kwamba watu wenye ualibino hukubwa na mifumo mibaya Zaidi ya ubakuzi ikiwemo ukatili na mateso. Tangu mwaka 2010 kumekuwa na takriban visa 700 vya mashambulizi na mauaji ya watu wenye ualibino katika nchi 28 za afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na hivi ni visa tu vilivyoripotiwa.

Mlezi akimhudumia mtoto ambaye alitelekezwa huko Goma, Kivu Kaskazini nchini DRC. Mara nyingi watu wenye ulemavu wa ngozi wanakumbwa na vitisho na ukatili.
UN /Marie Frechon
Mlezi akimhudumia mtoto ambaye alitelekezwa huko Goma, Kivu Kaskazini nchini DRC. Mara nyingi watu wenye ulemavu wa ngozi wanakumbwa na vitisho na ukatili.

Maadhimisho ya siku hii

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani maadhimisho yameambataza na matukio mbalimbali na kuhudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo mrimbwende kutoka Afrika Kusini Thando Hopa, pia kumekuwepo na tukio maalumu kwenye mkutano wa 12 wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu ambako kijana mwenye umri wa miaka 16 mwenye ualibino kutoka nchini Tanzania Mwigulu Matonange muathirika wa ukatili dhidi ya watu wenye ualibino aliyekatwa mkono na kusaidiwa na mfuko wa umoja wa Mataifa wa waathirika wa utesaji kupatiwa mkono wa bandia.

Pia alikuwepo Lazarus Chigwandali mtu mwenye ualibino kutoka Malawi ambaye anatumia muziki wake kuleta mabadiliko. Kwa pamoja na mtaalamu husru wa haki za binadamu kuhusu haki za watu wenye ualibino wanasimama imara kupigania haki za binadamu zikiwemo za wenye ualibino.