WATU WENYE ULEMAVU

Mashindano ya Olympiki ya walemavu yang'oa nanga Tokyo  wakimbizi  hawakuachwa nyuma: UNHCR

Mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yameanza rasmi hii leo mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi.

WHO na IPC kushirikiana kuwasaidia wanamichezo walemavu

Shirika la Afya ulimwenguni WHO na shirika la kimataifa la walemavu IPC hii leo wametiliana saini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kukuza usawa na kuheshimu tofauti zilizopo baina ya watu katika mipango inayohusu afya na michezo kwa kila mtu, kila mahali. 

Ulemavu sio kulemaa - Fahad na Ester wa Geita, Tanzania 

Watu wawili wenye changamoto ya uoni hafifu wanaoishi katika halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita Tanzania, wameungana kuanzisha mradi wa kutengeneza vyungu vya kupandia maua, kupikia na majiko ya udongo ili kuepuka utegemezi katika jamii kama yanavyohamasisha malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs.

Watu wenye ulemavu Burundi waamua kuutekeleza wito wa UN kwa vitendo 

Nchini Burundi, Dany Kasembe, mwenye ulemavu wa mguu, ameamua kuwashirikisha wenzake katika kuutekeleza wito wa Umoja wa Mataifa kwa vitendo, wito ambao unataka uwepo wa dunia ambayo watu wote wana uwezo wa kupata fursa sawa na pia ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika jamii ikiwemo katika hatua za kukabiliana na kujikwamua na janga la corona au COVID-19. 

Ujumuishaji wa watu wenye ulemavu ni haki ya msingi ya binadamu:Guterres

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa amesema wakati dunia ikijikwamua kutoka kwenye janga la COVID-19 ni lazima kuhakikisha kwamba matarajio na haki za watu wenye ulemavu zinajumuishwa na hilo litatimia tu endapo watu hao watashirikishwa na kuwakilishwa ipasavyo. 

Ili kufanikisha malengo yetu lazima tuwajumuishe watu wenye ulemavu:UN

Kuwa na dunia ambayo watu wote wana uwezo wa kupata fursa saw ani lengo ambalo linastahili kupiganiwa amesema Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa katika hotuba yake hii leo akitoa wito wa ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika jamii ikiwemo katika hatua za kukabiliana na kujikwamu na janga la corona au COVID-19.

Djenalib Ba: Ulemavu unakuwa kulemaa kutokana na fikra za watu

Watu bilioni 1 kote dunia wana ulemavu na asilimia 80 wanaishi katika nchi zinazoendelea wakikabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo unyanyapaa, ubaguzi na kutopata fursa za kuwezesha kuchangia katika jamii kwa mujibu wa shirika la kimataifa la mpango wa maendeleo ya kilimo IFAD.  Nchini senegali mm

Sauti -
2'12"

Ulemavu unakuwa kulemaa kutokana na fikra za watu: Djenalib Ba

Watu bilioni 1 kote dunia wana ulemavu na asilimia 80 wanaishi katika nchi zinazoendelea wakikabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo unyanyapaa, ubaguzi na kutopata fursa za kuwezesha kuchangia katika jamii kwa mujibu wa shirika la kimataifa la mpango wa maendeleo ya kilimo IFAD.  Nchini senegali mmoja wa watu wenye ulemavu ameamua kukabiliana na moja ya fikra potofu kwamba ulemavu ni kulemaa. Kulikoni? 

Guterres:Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja

Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.

Sauti -
1'25"

06 Mei 2020

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa  tunaangazia habari tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani:

Sauti -
11'18"