Mfumo waanzishwa kudhibiti uvuvi wa kupindukia wa samaki

19 Februari 2018

Umoja wa Mataifa umeanzisha mfumo wa aina yake ya kubadilishana taarifa za uvuvi kama njia mojawapo ya kudhibiti uvuvi wa kupindukia unaohatarisha uwepo wa samaki duniani.

Kituo cha uwezeshaji biashara cha Umoja wa Mataifa kimesema biashara ya samaki inakadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 140, lakini biashara hiyo iko hatarini kutokanana uvuvi wa kupindukia na uvuvi haramu.

Katika taarifa yake kituo hicho kimesema hali inakuwa mbaya zaidi kwa kuwa ripoti zozote kuhusu mienendo ya uvuvi zipo kwenye karatasi na kufanya vigumu nchi au taasisi kuweza kuzipata na kufuatilia.

Ni kwa mantiki hiyo wameanzisha mfumo wa kisasa wa kubadilishana taarifa  kama vile vyombo vya uvuvi, mienendo yao ya safari, takwimu kuhusu samaki, leseni na takwimu za ukaguzi,  mfumo ambao utasaidia kulinda maeneo ambayo tayari samaki wamepungua.

Kituo hicho kinasema mpango huo unakwenda sambamba na lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambalo pamoja na mambo mengine linataka uvuvi endelevu na usioharibu mazingira.

Tayari Muungano wa Ulaya umeanza kuzingatia mfumo huo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter