WFP yafikiria kusitisha utoaji misaada sehemu zinazodhibitiwa na Houthi nchini Yemen

21 Mei 2019

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linataka mambo matatu ya dharura kufanyika nchini Yemen yakiwemo: uhuru wa kuhudumu, kuwafikia wale walio na njaa na kufanyika usajili wa kieletroniki.

Katika taarifa yale iliyotolewa leo WFP imesema  imebaini kwamba chakula cha msaada nchini Yemen mwezi Desemba mwaka 2018 kilipelekwa kwingine hasa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa kundi la Houthi.

Kufuatia hali hiyo WFP ilimeuandikia uongozi wa Houthi nchini Yemen na keuelezea hatua zinazohitajika kuchukuliwa ili kuhakisha kuwa utoaji wa chakula unafikia viwango vya kimataifa nchini humo na unawafikia walengwa.

WFP imeomba ruhusa kutoka kwa mamlaka ikitaka kuwachagua wale wanaonufaika na misaada na kuanza mfumo wa usajili ambao utaiwezesha  WFP kutambua sehemu zinazokumbwa na njaa na kuzifikia.

Kati ya mwisho mwa Desemba 2018 na Machi 2019, WFP imekaribisha hatua zilizopigwa katika suala hilo, lakini tangu mwezi Machi mwaka huu, ushikiano unaonekana kukwama.

 Mapema Mei mwaka huu  mkurugenzi mkuu wa WFP aliwaandikia tena Houthi akielezea wasiwasi kwa kutokuwepoa na hatua zilizochukuliwa akisema kuwa ikiwa hatua muafaka hazitakuwepo, WFP itatathmini kusitisha oparesheni zake katika sehemu zilizo chini ya udhibiti wa Houthi nchini Yemen.

TAGS:Houthi, Yemen, WFP, msaada wa chakula, wakimbiz

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud