18 JUNI 2021
Katika jarida la mada kwa kina la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea
-Mamilioni ya wakimbizi kuendelea kukabiliwa na njaa endapo msaada wa fedha za msaada hautopatikana limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP
-Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema inatiwa wasiwasi miubwa na kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao kwenye jimbo la Marib nchini Yemen, mashambulizi yanayofanywa na kundi la Houthi