Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 50 kutoka Kuwait kuwezesha WFP kupeleka chakula Yemen

Usambazaji wa misaada nchini Yemen.(Picha:WFP)

Dola milioni 50 kutoka Kuwait kuwezesha WFP kupeleka chakula Yemen

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limekaribisha hii leo mchango wa dola milioni 50 kutoka Kuwait kwa ajili ya msaada wa dharura wa chakula  kwa zaidi ya watu milioni 2.9 nchini Yemen.

 Mageed Yahia ambaye ni mkurugezi wa WFP kwa nchi za Falme za kiarabu na zile za ghuba, amesema mchango huo kutoka kwa Sheikh Sabah Al-Ahmed A Jaber-Al Sabah mfalme wa Kuwait, utasaidia kufikisha chakula kwa familia mbalimbali za waathirika katika mgogoro unaoendelea nchini Yemen.

WFP inasema vita vya zaidi ya miaka mitatu vinavyoikabili Yemen, vimesababisha zaidi  ya watu milioni 18 kutokuwa na uhakika wa mlo na milioni 8 kati yao wanaishi katika umasikini wa kupindukia na hutegemea msaada wa mashirika ya kibinadamu kwa mahitaji ya chakula.

Naye Stephan Anderson ambaye ni mkurugenzi wa wa WFP Yemen amesema mchango huu kutoka serikali wa Kuwait  umekuja wakati muafaka na utawezesha shirika hilo kuendelea kuwapatia msaada wa chakula wananchi wenye uhitaji na kwamab hakuna mtu anayepaswa kubaki bila chakula.

Amesema pindi mtoto mmoja anapofariki dunia kila baada ya dakika 10 nchini Yemen ktokana na magonjwa yanayoweza kuepukika, suluhisho pekee la kuokoa maisha ni kumaliza mapigano na kumaliza njaa.
Kuwait ni moja ya wasaidizi wakubwa wa misaada ya kibinadamu na maendeleo ya WFP duniani kote.

Katika 10  iliyopita, Kuwait imechangia karibu milioni 190 za Marekani kwa shughuli za WFP kimataifa, na kusaidia katika kupunguza njaa kwa watu wengine walioathirika zaidi duniani.

Usaidizi huo ulitangazwa na mwakilishi wa kudumu wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa, Balozi Mansour Al Otaibi .