Baraza la Usalama lalaani shambulio Mali

19 Mei 2019

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani shambulio la tarehe 18 mwezi huu dhidi ya walinda amani nchini Mali.

Katika taarifa yao iliyotolewa leo mjini New York, Marekani, wajumbe hao wametuma
Salamu za rambirambi kwa serikali ya Nigeria na familia ya mlinda amani ambaye aliuawa kwenye shambulio hilo lililofanyika huko Timbuktu na Tessalit ambapo pia walinda amank wengine walijeruhiwa.

Wajumbe hao pia wametoa wito kwa serikali ya Mali kuchungjza kwa kina shambulio hilo na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Wamesisitiza kwamba mashambulio yoyote dhidi ya walinda amani yanaweza kuwa uhalifu wa kivita kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Wajumbe hao wamesisitiza kuwa ushiriki katik kupanga, kuongkza au kufadhili mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSCA, unachangia kuweza kuwekewa vikwazo vya Baraza la Usalama.

Wajumbe hao wamesisitiza kuwa ugaidi katika aina zote ni moja ya tishio la amani na usalama duniani na wamesisitiza kuwa watekelezaji, wafadhili wa vitendo hivyo wafikishwe mbele ya sheria.

Halikadhalika wamesema wanaunga mkono juhudi za mwakilishi maalum wa UN nchini Mali, na harakati zote za kuleta amani nchini Mali.
 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter