Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti  na maendeleo kutatua changamoto za afya:WHO

Mradi wa IAEA wa kusaidia tiba dhidi  ya saratani katika nchi za kipato cha chini na kati umesaidia mataifa kutekeleza mipango mahsusi ya kutibu saratani
IAEA
Mradi wa IAEA wa kusaidia tiba dhidi ya saratani katika nchi za kipato cha chini na kati umesaidia mataifa kutekeleza mipango mahsusi ya kutibu saratani

Utafiti  na maendeleo kutatua changamoto za afya:WHO

Afya

Leo, Idara mpya ya sayansi ya shirika la afya ulimwenguni ,WHO imezindua rasilimali  muhimu mtandaoni ili kutoa muongozo wa kutengeneza  bidhaa mpya za afya ambazo zina masoko madogo au motisha kwa ajili ya utafiti na utengenezaji  wa bidhaa za tiba pamoja na maendeleo.

Ikiwa ni nyenzo muhimu kwa kuhakikisha huduma ya afya kwa wote duniani muongozo huo unalenga kuchagiza utafiti na uutengenezaji wa bidhaa zitakazopambana na magonjwa yaliyopuuzwa na vitisho vya afya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na usugu wa vijiumbe maradhi na magonjwa ambayo yana uwezekano wa kuzusha janga kubwa.

Nyenzo hiyo ambayo inaelezea na kuorodhesha bidhaa za afya ni bure kuitumia mtandaoni ambayo imeandaliwa na mpango maalumu wa utafiti na mafunzo ya magonjwa ya Kitropiki (TDR) kwa niaba ya WHO.

Nyenzo hiyo inatoa fursa ya kurambaza maelezo ya bidhaa za afya ambazo zinahitajika kushughulikia masuala ya afya ya kimataifa ikiwemo yale yaliyopewa kipaumbele na WHO.

Orodha ya nyezo hiyo inafafanua kuhusu masuala 8-10 kama vile jamii lengwa, hatua za kuchukua na kiwango cha dawa, kwa ajili ya kuunda dawa, chanjo, na vifaa ya uchunguzi.

WHO inasema kuzingatia masuala haya katika hatua za mwanzo za mchakato wa maendeleo ni muhimu sana ili kuahakikisha bidhaa kamili zitakazozalishwa zinapatikana kwa watu wanaozihitaji. Iikitoa mfano wa mlipuko wa karibuni wa Ebola 2014-2015-umeainisha haja ya haraka ya kuwa na taarifa ili kutoa muongozo na kuimarisha uratibu wa juhudi za kutengeneza bidhaa mpya za afya kwa magonjwa yaliyopuuzwa na kwa watu yanayowaathiri.

Kifaa kinachotumiwa kwa chanjo dhidi ya kifua kikuu TB.Chanjo inatayarishwa  katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.
© UNICEF/Ilvy Njiokiktjien
Kifaa kinachotumiwa kwa chanjo dhidi ya kifua kikuu TB.Chanjo inatayarishwa katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.

Mchango ni wa kila mtaalamu

Kwa mujibu wa mwanasayansi mkuu wa WHO Dkt. Souya Swaminathan nyenzo hii mpya iliyozinduliwa itasaidia kuchagiza na kusambaza ajenda ya shirika hilo kuhusu utafiti ili kuweza kufikia huduma za afya kwa owte.”Wakati orodha hiyo imezinduliwa ikijikita kwa magonjwa ya kuambukiza tunaendelea kukuza orodha yetu na kupanua wigo wa mada tunazoweka , hivyo nakaribisha uwasilishaji wa orodha za bidhaa  zingine ambazo ni za maeneo yanayopewa kipaumbele kama magonjwa yasiyo ya kuambukiza na usugu wa vijiua vijiumbe maradhi.”

Hivi sasa nyezo hiyo ya mtandaaoni ina orodha ya bidhaa 196 zilizotengenezwa na mashirika 24 ambapo 191 kati hizo zimeelezewa kuwa zinalenga  magonjwa ya kuambukiza . Na magonjwa manne yaliyopewa kipaumbele katika bidhaa hizo ni kifua kikuu, malaria, HIV na ukimwi na Chagas ugonjwa ambao unatokana na kuumwa na wadudu ana ambao unaweza kusamabisha kuvimba, homa na usipotibiwa huleta maradhi ya moyo kushindwa kufanya kazi.