Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Salame ahuzunishwa na mgawanyiko ndani ya Baraza la Usalama, WHO yaimarisha huduma za afya

Daktari katika matibabu ya mtoto wa umri wa miaka minne nchini Libya ambapo yaelezwa kuwa mzozo ukiendelea hosptiali zinakabiliwa na mzigo mkubwa.
WHO
Daktari katika matibabu ya mtoto wa umri wa miaka minne nchini Libya ambapo yaelezwa kuwa mzozo ukiendelea hosptiali zinakabiliwa na mzigo mkubwa.

Salame ahuzunishwa na mgawanyiko ndani ya Baraza la Usalama, WHO yaimarisha huduma za afya

Wahamiaji na Wakimbizi

Idadi ya watu waliouawa katika siku 24 zilizopita kufuatia mapigano yanayoendelea kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli na viunga vyake imefikia 345 huku majeruhi ni 1652.

Msemaji wa shirika la afya ulimwenguni, WHO, Tarik Jasarevic amesema hayo leo wakati huu ambapo mwakilish maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wataifa nchini Libya Ghassan Salamé, anaelezea machungu yake kutokana na mgawanyiko mkubwa ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mgawanyiko ambao amesema umekwamisha harakati za kusitisha mapigano hayo.

Salamé amenukuliwa na chombo kimoja cha habari nchini Ufaransa akisema kuwa “mgawanyiko huo ndani ya Baraza la Usalama umekwamisha azimio lililoandaliwa na Uingereza lenye lengo la kusitisha mapigano. Miaka minane tangu kuondolewa madarakani kwa Muammar Gaddafi, Libya bado haina utulivu wa kisiasa,”

WHO inasema hivi karibuni ilipeleka jopo lingine la dharura la wataalamu wa afya likiwa na vifaa vya upasuaji.

“Hivi sasa tuna timu zetu zinazofanya kazi kwenye hospitali tatu ambazo zinapokea majeruhi. Katika wiki tatu zilizopita, timu hizi za upasuaji zimefanya operesheni kubwa zaidi ya 140 na operesheni  nyingine ndogo 1oo,” amesema Bwana Jasarevic.

WHO inasema kwa kuzingatia kuwa kuna takribani wakimbizi wa ndani 40,000, shirika hilo limethamini mahitaji ya vituo vya afya karibuni na makazi ya wakimbizi hao wa ndani na hivis sasa inasaidia kuvipatia vifaa vya matibabu ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao wa ndani.