Hali Libya sio endelevu na taifa linaendelea kuyumba: Salame

16 Julai 2018

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesema ingawa kuna hatua zilizopigwa katika kurejesha utulivu nchini humo, machafuko ya hivi karibuni yanaonyesha kwamba bado kunahitajika hatua zaidi ili kuepuka zahma ya kiuchumi na kisiasa.

Ghassan Salame ameyasema hayo leo kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani wakati alipowasilisha ripoti kuhusu hali nchini Libya.

Bwana Salame amsema mazungumzo yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Libya yamechangia kupungua kwa machafuko na kuongezeka kwa majadiliano mwaka 2018 kupitia mazingira yaliyoundwa kwa ajili ya makubaliano ya maridhiano , ingawa ameongeza kuwa sio habari zote ni Njema.

 

UN /Eskinder Debebe
Ghassan Salamé, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL akihutubia Baraza la Usalama kwa nija ya video kutoka Tripoli,Libya

Ameongeza kuwa ingawa sehemu ya kwanza yam waka huu kwa kiasi kikubwa kumekuwa na utulivu kutokana na udhibiti wa hatua zajeshi , lakini miezi miwili iliyopita ilighubik,wa na matukio ya ghasia.

“Idadi ya raia waliouawa ilipungua hadi kufika wane mwezi Machin a watano mwezi Aprili” amesema Salame ambaye ripoti yake ameiwasilisha kwa njia ya video kutoka mjini Tripoli ambako mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umerejea rasmi katika operesheni zake na hivi karibuni utafungua ofisi mjini Benghazi.

Salame ameeleza kwamba awamu ya majadiliano ya mkutano wa kitaifa imekamilika kwa mafanikio, ikiwa ni sehehemu  ya mpango wa hatua wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya.

Hatua hiyo imehusisha mikutano Zaidi ya 75, washiriki 70,000 raia wa Libya wakiwemo wanawake, wakimbizi wa ndani, vijana na wajumbe wa jamii zilizotengwa za Kusini mwa nchi hiyo.

UNICEF/Alessio Romenzi
Wahamiaji wakiwa wamelala kwenye magodoro kwenye moja ya vituo vya kushikilia wahamiaji huko nchini Libya.

Ameongeza kuwa “hii ilikuwa ni mara ya kwanza jamii hizo kujumuishwa katika majadiliano kuhusu mchakato wa kisiasa wa kujenga, mustakhbali wa taifa hilo.”

ONGEZEKO LA MACHAFUKO

Kwa salame, mchakato wa kisiasa unauhusiano wa moja kwa moja na kutokuwepo kwa shughuli za kijeshi , hali ambayo imeonekana dhahiri katika miezi miwli ya mapigano kwenye mji wa Derna ambako raia ndio waathirika wakubwa na hofu yake ni kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji na watu kukamatwa kiholela.

Ametoa wito kwa pande zote kuheshimu sharia za kimataifa za kibinadamu.Amesema jeshi la serikali lilipigana kufa na kupona kuchukua udhibiti wa mji wa huo, ingawa hilo tayari limefanikiwa bado na machafuko yanayozuka mara kwa mara .

“Kuporomoka kwa uchumi, kusambaratika kwa huduma za umma na kuzuka kwa machafuko mara kwa mara , serikali haiwezi kuwa endelevu nan chi inapoteza dira” Amesema.

Pia ameonya kwamba magaidi wa Lurk Libya, wahalifu wanaosubiri kusafirisha kiharamu wahamiaji, ongezeko la mamluki wa kigeni na sekta ya mafuta kuwa katika hatihati , haya ni lazima yaitie hofu dunia nzima.

UCHAGUZI

Kuhusu uchaguzi Salame ameeleza kwamba umefanyika kwa njia ya Amani na tume ya uchaguzi inashughulikia masuala ya usalama ili kuendelea kuhakikisha chaguzi huru, jumuishi na salama.

Hata hivyo ameonya kwamba ingawa Libya inataka kuondokana na taasisi za sasa, endapo mazingira muafaka hayatokuwepo, itakuwa haina maana kuendesha uchaguzi.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud