Asasi za kiraia zachagiza SDGs nchini Tanzania

24 Januari 2019

Tanzania ikijiandaa kuwasilisha mwaka huu Umoja wa Mataifa ripoti yake ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, jukwaa la maendeleo endelevu nchini humo limeanzisha utaratibu wa jinsi ya kujumusha mawazo ya wanachama wa jukwaa hilo ambao ni asasi za kiraia.

Steven Chacha mwanzilishi mwenza wa Tanzania Data Lab na wenyeji wa jukwaa hilo amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC nchini Tanzania.

“Tumeanzisha utaratibu mahsusi kwa ajili ya asas iza kiraia kuweza kufautilia. Na mawazo haya tunataka tuyakusanye kutoka ngazi zote. Na tunamulika malengo yote 17 ya maendeleo endelevu.  Ili kuweza kupata mrejesho kutoka asasi hizo kuwa ni nini ambacho tumeweza kufanya katika ngazi ya mtaa, kijiji, kata, wilaya mkoa hadi taifa. Na pia tunaonaje taswira ya nchi katika utekelezaji wa malengo hayo ambayo ripoti yake ya utekelezaji itawasilishwa Umoja wa Mataifa mwaka huu.”

Bwana Chacha akaelezea maeneo ambayo asasi za kiraia zimejikita zaidi..

“Idadi kubwa sana ya asas iza kiraia zimejikita kwenye maeneo ya kuondoa umaskini, afya, elimu, upatikanaji wa maji safi na salama na hayo ndio maeneo makuu ambayo asasi nyingi zimejikita. Tuna mapungufu makubwa sana kwenye maeneo kama mazingira. Idadi ya asasi za kiraia zinazofuatilia masuala ya mazingira bado ni ndogo. Malengo mengi yanayohusiana na mazingira, uwepo wa asasi za kiraia ni ndogo sana. Pia kwenye viwanda, bado kuna asasi chache sana zinazojishughulisha na kufuatilia maeneo hayo.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter