Elimu ni muhimu katika kuhakikisha misitu endelevu -FAO

21 Machi 2019

Ikiwa leo Machi 21 ni siku ya misitu duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limesisitiza umuhimu wa kuchagiza elimu kuhusu kupenda misitu.

FAO katika ujumbe wake wa mwaka huu kwa siku hii imetaja umuhimu wa elimu katika nyanja zote kwa ajili ya kufikia misitu endelevu na inayojali bayoanuai. Kwa mujibu wa FAO, misitu yenye afya, inachangia katika kujenga jamii zenye ustahimilivu na uchumi imara. Akisisitiza hoja hiyo Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Kenya, Gabriel Rugalema amesema uhifadhi wa misitu hususan Afrika Mashariki ambako jamii zinategemea misitu kwa ajili ya kuendesha maisha yao ikiwemo matumizi ya kuni na mkaa bado unasuasua lakini baadhi ya jamii zimeanza kuchukua hatua

(Sauti ya Rugalema)

Bwana Rugalema amekwenda mbali zaidi akielezea wajibu wa serikali na mashirika kutoa miche kwa wakulima kwani.

(Sauti ya Rugalema)

 FAO imesisitiza kwamba uhifadhi wa misitu ni muhimu wakati idadi ya watu duniani ikitarajiwa kufika bilioni 8.5 kifikapo mwaka 2030.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter