Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya maziwa nchini Kenya ni muarobaini wa kutokomeza njaa na kuzalisha ajira- FAO

Maziwa yanauwezo wa kuboresha lishe ya dunia maskini
Picha EADD/Neil Thomas/FAO
Maziwa yanauwezo wa kuboresha lishe ya dunia maskini

Sekta ya maziwa nchini Kenya ni muarobaini wa kutokomeza njaa na kuzalisha ajira- FAO

Ukuaji wa Kiuchumi

Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO nchini Kenya limezungumzia jinsi uwekezaji katika sekta ya maziwa kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki,umekuwa muarobaini katika siyo tu kuchagiza kuondokana na njaa bali  pia kuimarisha kipato.

Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Kenya, Gabriel Rugalema amesema hayo wakati akihojiwa na Abdikarim Said Haji wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC mjini Nairobi, Kenya ambapo amesema..

“ Ukiangalia hiyo sub-sekta ya Dairy, uzalishaji wa maziwa , ni kubwa sana.  Wakulima wanafuga mifugo, watu wananunua maziwa, wengine wanasafirisha maziwa.Makampuni mengine yanazalisha Cheese, mengine yanazalisha Yoghurt na mengine yanazalisha vitu vingine ,kwa hivyo Kenya katika Afrika imefanya vizuri kwenye hii sekta na tungependa iendelee kufanya vizuri, lakini vilevile ni mfano wa kuigwa vilevile na nchi za jirani kwa sababu inaweza ikaleta fedsha nyingi na ikaleta ajira kubwa na ikaleta lishe nzuri.”

Ufugaji mzuri wa ng'ombe ni moja  ya miradi inayokomboa wakazi kwenye nchi ambazo zimewekeza vizuri katika sekta hiyo
Patrick Zachmann/Magnum Photos for FAO
Ufugaji mzuri wa ng'ombe ni moja ya miradi inayokomboa wakazi kwenye nchi ambazo zimewekeza vizuri katika sekta hiyo

Bwana Rugalema alipoulizwa ni mambo yapi ambayo Kenya inaweza kujivunia katika kuboresha sekta ya kilimo na kutokomeza njaa kiasi kwamba nchi nyingine zinaweza kujifunza ni kubuniwa kwa apu za kuwezesha wakulima kupata masoko, kufahamu utabiri wa hali  ya hewa na pia kupata pembejeo lakini zaidi ni mgao wa fedha kwa familia zisizo na uwezo wa kujikimu akisema.

“ Nadhani hiyo nayo ni suala muhimu hasa kwa nchi za Afrika ambako bado kuna umaskaini sana. Hiyo Programu bado iko kwenye vijiji, lakini kumbuka upungufunwa chakula hauko tu vijijini isipokuwa vilevile katika familia za mijini hasa mabzo hazina kipato au kipato kidogo sana kwa hiyo na hiyo tunategemea itakwenda mpaka  kwenye famila za mijini.”