Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika kuadhimisha siku ya misitu FAO yazindua mpango mpya kwa ajili ya misitu na maji:

Katika kuadhimisha siku ya misitu FAO yazindua mpango mpya kwa ajili ya misitu na maji:

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO limezindua mpango mpya kwa lengo la kuongeza fursa ya umuhimu wa misitu katika kuboresha hadhi ya maji na upatikanaji wake , katika wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya misitu.

Mpango huu utajikita zaidi katika uhusiano baina ya misitu na maji na utaanza kwa kuangalia njia za kuboresha usalama wa maji katika nchi nane za Afrika ya Magharibi ambazo ni Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Sierra-Leone.

FAO itafanya kazi kwa karibu na jamii husika ili kuongeza uelewa wao wa mwingiliano kati ya misitu na maji na kuwasaidia kuunganisha usimamizi wa misitu katika mazoea yao ya kilimo ili kuboresha usambazaji wa maji.

FAO inatumia siku ya misitu mwaka huu kutanabaisha jinsi misitu inavyoweza kuchangia kuimarisha upatikanaji wa maji hususani katika nchi ambazo zinakabiliwa na uhaba wa bidhaa hii muhimu.