WHO yajizatiti kuitokomeza TB inayoua watu 4500 kila siku.

20 Machi 2019

Kuelekea siku ya kifua kikuu itakayoadhimishwa tarehe 24 mwezi huu, Shirika la afya duniani WHO hii leo mjini Geneva Uswisi limetoa mwongozo mpya wa jinsi ya kuboresha matitabu ya ugonjwa wa kifua kikuu kilicho sugu kwa dawa zinazoaminika (MDR-TB). WHO inasema matibabu mapya ni bora zaidi na yana kiwango kidogo cha kuweza kusababisha madhara ya baada ya matumizi.

Pia shirika hilo linapendekeza matumizi ya dawa hizo kwa kufuata usalama wa dawa na pia kuwasaidia wagonjwa na kuwapa ushauri wa kuwasaidia kumaliza dozi ya matibabu yao.

Mapendekezo haya mapya , ni sehemu ya mkusanyiko wa hatua zilizoandaliwa ili kusaidia nchi kuongeza kasi katika maendeleo ya kutokomeza TB.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, “kaulimbiu ya mwaka huu ya siku ya TB duniani :” Ni wakati wa kukikotokomeza Kifuu Kikuu. Tunasisitiza umuhimu wa kutekeleza ahadi zilizofikiwa mwaka 2018 katika mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kifua Kikuu katika kuchukua hatua za kuhakikisha kila mmoja anayehitaji matibabu ya kifua kikuu anayapata.”

Taarifa ya WHO inayopatikana pia katika tovuti ya shirika hilo inasema tangu mwaka 2000, maisha ya watu wapatao milioni 54 yameokolewa na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu vimepungua kwa theluthi moja. Lakini inaendelea kufafanua kuwa bado watu milioni 10 wanaugua kifua kikuu kila mwaka.

Mpango wa WHO umeundwa kuzisaidia nchi kuondoa mapungufu katika huduma ili kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma. Mambo muhimu ni pamoja na, mfumo wa uwajibikaji wa kuratibu hatua katika sekta na kufuatilia na kuchunguza maendeleo, kuzisaidia nchi kufahamu zaidi milipuko ya ugonjwa ndani ya nchi husika kwaa muda muafaka kwa kutumia mifumo ya uchunguzi ya kielekroniki pia mwongozo wa ufanisi bora wa kupanga na utekelezaji wa hatua za TB kulingana na uchambuzi wa njia za mgonjwa katika kupata huduma.

Tarehe 22 Machi, washirika wakuu watakusanyika kwenye mkutano wa Siku ya Kifua kikuu katika ofisi za WHO huko Geneva ili kuharakisha hatua za kumaliza kutokomeza kifua kikuu. WHO itawasilisha mwongozo huo mpya katika mkutano huo.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

WHO yazindua njia mpya za kupima na kutambua kwa haraka ugonjwa wa kifua kikuu

Shirika la afya duniani WHO limeanzisha njia mpya a kupima ugonjwa wa kifua kikuu ambayo itawezesha kujulikana kwa mgonjwa anyeugua ugonjwa huo kwa muda wa takriban dakika 100 kinyume na sasa ambapo ugonjwa huo unachukua karibu miezi mitatu kujulikana.

Siku ya Kupiga Vita Maradhi ya Kifua Kikuu/TB Duniani

Tarehe ya leo ya Machi 24 huheshimiwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Maradhi ya Kifua Kikuu/TB Duniani. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) thuluthi moja ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wameambukizwa na maradhi ya TB.