Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Afrika Mashariki na namna wanavyoleta mbadiliko katika jamii

Washiriki wa tukio la kuchagiza usawa wa kijinsia katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani mjini New York.
Photo: UN/Radmilla Suleymanova
Washiriki wa tukio la kuchagiza usawa wa kijinsia katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani mjini New York.

Wanawake Afrika Mashariki na namna wanavyoleta mbadiliko katika jamii

Wanawake

Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake duniani masuala mengi yameangaziwa, ikiwemo umuhimu wa kumwezesha mwanamke lakini suala ambalo ni la msingi na wakati mwingine halimulikwi ni mchango wa wanawake wenyewe katika kujikwamua na hata kuikwamua jamii kupitia shughuli wanazozifanya.

Ni kwa kuzingatia hilo ambapo leo tunamulika wanawake watatu kutoka nchi za Afrika Mashariki. Licha ya kuwa wametoka nchi tofauti lakini wanawake hawa wamejizatiti kuboresha sio tu maisha yao bali pia kuinua jamii zao kwa ujumla kwa kutumia mbinu mbalimbali.