Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

CBD

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC FAO kwa ushirikiano na wadau wamefanya ufuatiliaji wa aina za miti kwenye misitu, ikiwa ni mara ya kwanza.
©FAO

Tumecheza tungo ya vurugu, sasa tuchukue hatua mtambuka kulinda sayari dunia- Guterres akiwa COP15

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati huu ambao wakazi wa dunia wanaongeza kasi ya vita dhidi ya mazingira ya sayari dunia, ni wakati muafaka kwa washiriki wa mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu bayonuai, CBD, COP15 wapitishe mkataba wa kujenga maafikiano yenye matarajio makuu na sayari dunia ili hatimaye kuacha dunia ya  bora, ya kijani na endelevu zaidi kwa vizazi vijavyo.

UNDP/Ya'axche

Tusipolinda bayoanuai tunajiangamiza wenyewe:CBD

Tatizo la kutoweka kwa bayoanuai ambayo ni muhimili mkuu wa maisha ya dunia na viumbe vilivyomo linaongezeka kila uchao na mlaumiwa mkubwa ni binadamu na shughuli zake za kila siku. Mwishoni mwa wiki Dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya bayoanuai iliyobeba kaulimbiu  “sisi ni sehemu ya suluhu”  Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa kila mtu kuwajibika kuilinda bayoanuai ambayo hakuna atakayesalimika bila hiyo .

Sauti
9'5"

24 MEI 2021

-Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Leah Mushi anakuletea 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo mjni Goma jimboni Kivu Kaskazini umesababisha vifo vya watu 15. 

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Shirika la afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni, WHO na kusema iwapo ubaguzi katika utoaji chanjo dhidi ya COVID-19 utaendelea, nchi tajiri zitachanja watu wake  huku virusi vikiendelea kusambaa  katika nchi

Sauti
11'10"
Homa ya nguruwe ambayo inaambukiza sana na inaweza kuwa na athari kubwa kwa wafugaji wadogo. (Maktaba Machi 2017)
IAEA/Laura Gil Martinez

Virusi visivyojulikana vipatavyo 850,000 viko kwa wanyama na ndege na vinaweza kuathiri binadamu :IPBES/CBD Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa leo na jukwaa la kimataifa la sera za kisayansi kuhusu bayoanuai na huduma za mifumo ya viumbe (IPBES) na kutathiminiwa na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya bayoanuai (CBD), imeonya kwamba majanga makubwa ya milipuko ya magonjwa yako njiani laki hatua madhubuti zikichukuliwa hatari inaweza kupunguzwa.

Sauti
5'57"