Dau la plastiki, Flipflopi safarini kutoka Kenya hadi Zanzibar

25 Januari 2019

Hatimaye dau la plastiki limeanza safari yake ya kilometa 500 kutoka Mombasa Kenya hadi Zanziabar Tanzania. Tumezungumza na mjenzi wake Ali Skanda

Dau lililotengenezwa kwa taka za plastiki likiwa safarini kutoka Lamu Mombasa nchini Kenya likielekea Mji Mkongwe huko Zanzibar nchini Tanzania, mjenzi wa dau hilo Ali Skanda amezungumzia lengo la safari hiyo iliyoanza jana na inatarajiwa kumalizika ndani ya siku 12 hadi 14. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Dau hilo la plastiki likipatiwa jina la FlipFlopi kutokana na kandambili chakavu kutumika pia katika kutengeneza, linasafiri kilometa 500 kueneza ujumbe wa mapinduzi ya plastiki kwa wakazi wa pwani ya Tanzania na Kenya.

Ujenzi wake umetumia zaidi ya tani 10 ambapo tulimuuliza mjenzi wake Ali Skanda, sababu hasa ya ujenzi wa boti hii ya plastiki.

"Nilitembelewa na rafiki yangu Ben Morrison ambaye alikuwa na hili wazo la kutengeneza boti la plastiki. Na sisi tulikuwa tunaumia sana kuoana jinsi ambavyo takataka zinatupwa hovyo baharini."

 

Bwana Skanda akaelezea kile ambacho ni ujumbe wake kwa wakazi wa Unguja ya kwamba waweke fuo zao katika mazingira safi na salama kwa kuwa plastiki ni hatari si tu kwa mazingira ya baharini bali pia viumbe vya baharini na binadamu.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Dau lilitengenezwa kwa mabaki ya taka za plastiki litasafiri kati ya miji mikongwe ya Afrika Mashariki.

Dau la kijadi lililotengenezwa na taka za plastiki zilizookotwa pwani ya Kenya na miji mbalimbali litaanza safari yake ya kwanza tarehe 24 mwezi huu kutoka mji mkongwe wa Lamu nchini Kenya hadi mji mkongwe huko Zanzibar nchini Tanzania tarehe 7 mwezi ujao, ikiwa ni safari ya umbali wa kilometa 500.