Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar

7 Februari 2019

Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya  kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini. 

Likiwa limebeba wanamazingira kutoka shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na kampuni iliyohusika na ujenzi, Flipflopi, dau hilo lilipata fursa kuhamasisha jamii hizo za pwani juu ya madhara ya plastiki.

Walikutana na wanafunzi, wanajamii na viongozi wa serikali na kubadilishana mawazo kuhusu jinsi ya kubadili mtazamo wa matumizi ya plastiki.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa baada ya dau hilo kutia nanga mji mkongwe, Mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini Tanzania, Clara Makenya amesema..

(Sauti ya Clara Makenya)

Na le lengo la safari limetimia

(Sauti ya Clara Makenya -2

Dau hilo lililojengwa na Ali Skanda kwa tani elfu 10 za taka za plastiki lilianza safari yake tarehe 24 mwezi Januari huko Lamu, nchini Kenya na kupitia Kipini, Malindi,Watamu, Kilifi, Mombasa, Diani, Shimoni, Wete, Pemba Kusini, Nungwi na hatimaye  leo  tarehe 7 limetia nanga Mji Mkongwe Zanzibar.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter