Baada ya vuta ni kuvute ya wiki mbili muafaka wafikiwa COP24

Baada ya wiki mbili za majadiliano ya makundi zaidi ya 200 yaliyokusanyika Katowice, Poland kwa ajili mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi , COP24 ,yameidhinisha muongozo wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mwaka 2015, wenye lengo la kupunguza ongezeko ka joto duniani kuwa nchini ya nyuzi joto 2 ikilinganishwa na viwango vya kabla ya wakati wa viwanda.
Taarifa kutoka Katowice, Poland, iliyotolewaleo, inasema kuwa mkataba umeridhiwa baada ya majadiliano ya usiku kucha na hatimae kukasikika shangwe na vigegele kumkaribisha rais wa mkutano wa COP24, Michal Kutyka, akifungua kikao cha mwisho ambacho kilihirishwa mara kadhaa.
Rais huyo katika hotuba yake amewashukuru wajumbe waliokuwa wanamsikiliza katika chumba cha mikutano kwa kile alichokiita, “ ustahamilivu” akiweka bayanakuwa usiku uliopita ulikuwa , “mrefu sana”.
Ukumbi ulijawa na kicheko baada ya televisheni kuba iliyokuwa chumbani kuonyesha mjumbe mmoja akipiga mwayo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabianchi, Patricia Espinosa, amesema kuwa , Katowice imeonyesha kuwa kwa mara nyingine tena mnepo wa mkataba wa Paris ambao ni ramani ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Bw. Guterres ambaye amegusia suala la athari za mabadiliko ya tabianchi kama moja ya mkakati wake muhula huu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Alihudhuria mkutano wa Katowice mara tatu katika kipindi cha wiki tatu zilizopita ili kuunga mkono majadiliano hayo, lakini kutokana na kuahirishwa kwa mara kadhaa alilazimika kuondoka kabla ya kikao cha mwisho kutokana na shughuli zingine zilizomsubiri mahala pengine.
Muongozo ulioidhinishwa leo ambao baadhi wanauita , kitabu cha sheria,una nia ya kuhimiza hatua madhubuti dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuwanufaisha watu wa tabaka zote hususan wale walioko hatarini.
Ufadhili wa mpango tekelezi dhidi ya tabianchi.
Moja wa kipengele cha, “azimio la Katowice’ ni mpango wa wazi ambao una nia ya kuleta kuaminiana kati ya mataifa kuhusu uhakika kuwa mataifa yote yanajihusisha katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi. Unatoa muongozo wa jinsi ambavyo kila nchi itakavyotoa taarifa za mpango wa kitaifa wa kupunguza hewa chafuzi.
Pia makubaliano yamefikiwa ya jinsi ya kuangalia uwiano katika kipimo cha utoaji wa hewa chafuzi na endapo mataifa maskini yanahisi hayawezi kufikia viwango hivyo yafafanue ni kwa nini na ziainishe mpango wa kujenga uwezo wa kushughulikia hali hiyo.
Kuhusu ufadhili kutoka mataifa yaliyoendelea kusaidia yale ambayo bado ndio yananukia kuunga mkono hatua kuhusu tabianchi, mkakati unatoa mwanya wa lengo jipya kuanzia mwaka 2025 na kuendelea kutoka kukusanya dola bilioni 100 kwa mwaka lengo la sasa hadi 2020.
Hata hivyo kuna baadhi ya ibara ambazo wajumbe walitofautiana.
Mfano ibara ya sita inayohusu mfumo wa masoko ambao unazikubalia nchi kutimiza sehemu ya malengo yake ya ndani. Hii inafanyika kupitia uuzaji wa hewa ya ukaa ambapo mataifa yanakubaliwa kuuza sehemu yake ya utoaji wa hewa chafuzi.
Mkataba wa Paris unatambua umuhimu wa suala hilo wa kulinda hadhi za juhdi za mataifa mengi kutimiza sheria za kimataifa zinazotaka kuhakikisha kuwa kila tani ya hewa chafuzi inayotolewa inawajibishwa.
Hivyo ibara hiyo imebaki na imepangwa kujadiliwa katika mkutano uajo wa COP25 utakaofanyika nchini Chile.