Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini kwenye majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi-COP24

 Stanford Mwakasonda, afisa kutoka, UNEP anayehusika na kitengo cha kuzisaidia nchi zinazoendelea kutekeleza majukumu yao kama wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris,.
UN News/Yasmina Guerda
Stanford Mwakasonda, afisa kutoka, UNEP anayehusika na kitengo cha kuzisaidia nchi zinazoendelea kutekeleza majukumu yao kama wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris,.

Kuna matumaini kwenye majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi-COP24

Tabianchi na mazingira

Majadiliano ya mbinu za kupambana na mabadiliko ya tabianchi yanaendelea mjini Katowice nchini Poland huku washiriki wakionyesha matumaini ya azma ya mkutano huo wa 24 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi  au COP24.

Akizungumza na UN News kandoni mwa mkutano huo Stanford Mwakasonda, afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP anayehusika na kitengo cha kuzisaidia nchi zinazoendelea kutekeleza majukumu yao kama wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris, amesema ingawa bado kuna changamoto katika mjadiliano hayo, kuna nuru inayoangaza kizani

(SAUTI YA STANFORD MWAKASONDA)

Akifafanua kusu kinachofanywa na UNEP kuhakikisha nchi wanachama wanafikia azma hiyo ya kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi amesema

(SAUTI YA STANFORD MWAKASONDA CUT 2)

Mkutano huo uliowaleta pamoja wadau wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, wataalam, mashirika ya kimataifa, wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia na kuandaliwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mabadiliko ya tabianchi UNFCCC, utakunja jamvi kesho jumamosi ukitarajiwa kutoka na mikakati ya pamoja kusongesha mbele kimataifa juhudi za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi .

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.