Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya bora ni haki ya binadamu: Guterres

Mgonjwa Mzee apata huduma katika kituo kimoja cha utoajiwa huduma nchini Japan
WHO/Yoshi Shimizu
Mgonjwa Mzee apata huduma katika kituo kimoja cha utoajiwa huduma nchini Japan

Afya bora ni haki ya binadamu: Guterres

Afya

Afya bora ni haki ya msingi ya binadamu na kiungo muhimu cha kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu yaani SDGs ifikapo mwaka wa 2030.

Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika ujumbe wake katika maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote, ikiwa na kauli mbiu ya tuungane kwa huduma  ya afya kwa wote na wakati wa kuchukua hatua ni sasa”, amesema kuwa,uongozi imara na pia kuhusisha jamii ni muhimu kuhakikisha kuwa  watu wote wanapata huduma bora  wanazohitaji kuhusu afya zao.


Katibu mkuu amesema kuwa leo dunia inaadhimisha siku ya huduma za afya kwa wote duniani na hivyo huduma  bora za afya ya kiakili na  kimwili ni lazima ziwepo kwa kila mtu na popote pale, ingawa la kusikitisha ni kwamba hali sio hivyo kwa sababu  nusu ya idadi ya watu duniani hawapati huduma hizo.Ameongeza kuwa, “kila mwaka  watu milioni100 hutumbukia katika umaskini kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa zaidi ya kipato chao.”
Bw Guterres amesema hali hiyo haipaswi kumfika mtu yeyote na pia haistahili kuwa hivyo. Amesema  mataifa mengi duniani yamedhihirisha kuwa suala  la kutoa huduma bora za afya, linawezekana. Nchi hizo, ameendelea,kusema  “ zimeonyesha kuwa kuboresha huduama za afya ni njia moja ya kuwekeza katika nguvu kazi ambazo husaidia kukuza uchumi na hivyo kupunguza umaskini.”

Daktari akipima mgojwa wa kisukari India.
WHO/Atul Loke
Daktari akipima mgojwa wa kisukari India.


Hivyo ameshauri kuwa, uongozi imara na pia kujumuisha jamii ni vitu viwili muhimu vinavyosaidia kuhakikisha kuwa watu wote wanapata msaada wa matibabu ya kiafya wanayohiaji akisisitiza kuwa “Katika siku hii ya kimataifa hebu tuzingatie  azma yetu ya kuwa na dunia yenye huduma za afya kwa wote.”


Baraza kuu la umoja wa Mataifa Disemba 12 mwaka 2012 lilipitisha azimio la kuhimiza mataifa wanachama kuchapuza juhudi zao kuelekea utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wote- UHC- wakitaka, kila mtu, popote pale alipo, anapaswa kupata huduma bora anazoweza kama mkakati wa maendeleo ya kimataifa. Na tarehe hiyohiyo, 12 Disemba mwaka 2017, Umoja wa Mataifa , kupitia azimio namba 72/138, ukaitangaza siku hii kama siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote.

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.