Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watafiti wapazia sauti harakati za kuhifadhi udongo

Uhifadhi mzuri wa udongo ni muarobaini wa uzalishaji chakula bora duniani
FAO/Giuseppe Bizzarri
Uhifadhi mzuri wa udongo ni muarobaini wa uzalishaji chakula bora duniani

Watafiti wapazia sauti harakati za kuhifadhi udongo

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya udongo duniani, je wafahamu udongo unachafuliwa vipi? Na iwapo uchafuzi ukiendelea mustakhbali wa wakazi wa duniani u mashakani?

Leo ni siku ya udongo duniani ambapo Umoja wa Mataifa unataka kila mtu popote pale alipo kuacha uchafuzi wa udongo wakati huu ambapo theluthi moja ya udongo duniani unaotumika kwa ajili ya kuzalisha chakula umechafuliwa.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linasema shughuli nyingi za uchafuzi zinafanywa na binadamu kama vile kilimo kisichojali uhifadhi wa udongo, uchimbaji madini na utupataji holela wa taka.

Je nini kinafanyika kutunza udongo? Tunakwenda nchini Tanzania kwake Nicolaus Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM mkoani Kagera.

(Mahojiano)

FAO inaonya kuwa kadri idadi ya watu inavyokadiriwa kuongezeka na kufikia bilioni 9 mwaka 2050, kiwango cha uchafuzi wa udongo nacho kitaongezeka na hivyo kusababisha sumu kwenye chakula, maji ya kunywa na hewa inayovutwa na binadamu.

“Udongo una uwezo mkubwa wa kuchuja na kuzuia sumu au vichafuzi lakini uwezo huo una ukomo. Idadi kubwa ya vichafuzi vinatoka kwa binadamu,” imesema FAO ikisema angalau sasa maendeleo ya sayansi na teknolonia yanatia matumaini.

Kwa mujibu wa FAO, hivi sasa wanasayansi wana uwezo wa kubaini vichafuzi ambavyo si rahisi kuonekana kwa jicho la kawaida.

Ni kwa mantiki hiyo FAO inapatia msisistizo utekelezaji wa malengo namba 2,3,12 na 15 ambavyo kwa njia moja au nyingine  yanapigia chepuo matumizi sahihi ya rasilimali ya udongo ili hatimaye kuchagiza uhakika wa chakula.