AfCFTA ni muarobaini kwa kuunganisha Afrika- Kenya

21 Novemba 2018

Mkutano wa mwaka wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA ukiendelea huko Kigali, Rwanda kwa kuangazia utekelezaji wa makubaliano ya eneo huru la biashara barani Afrika, AfCFTA, Kenya imezungumzia sababu za kupatia kipaumbele eneo hilo huru la biashara.

 

Dkt. Julius Muia ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mipango nchini Kenya amesema hayo akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Umoja wa Mataifa mjini Kigali kandoni mwa mkutano huo akisema, "ili tukuze biashara katika Kenya lazima tuwe na ushirikiano na nchi nyingine katika Afrika na ndio Kenya ilikuwa nchi ya kwanza kuweka mkataba huu wa biashara huu katika Afrika"

Hadi sasa ni nchi 49 tu barani Afrika ndio zimesaini mkataba huo wa eneo la biashara huru barani Afrika huku ni 12 tu kati ya hizo ndio zimeridhia. 

ECA inasema kuwa mashauriano  yanaendelea ili kuangalia jinsi ya kufanikisha utekelezaji wa eneo hilo la biashara huru ya bidhaa na huduma ambapo kamisheni hiyo inatoa msada kiufundi kwa serikali katika awamu hizo za mazungumzo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter