Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Lagos hadi Kigali ndoto ya Afrika yatimia

Wachuuzi wa samaki kama hawa huko Mogadishu Somalia wanaweza kunufaika na eneo la biashara huru Afrika iwapo miundombinu sahihi itawekwa.
AU-UN IST/Stuart Price
Wachuuzi wa samaki kama hawa huko Mogadishu Somalia wanaweza kunufaika na eneo la biashara huru Afrika iwapo miundombinu sahihi itawekwa.

Kutoka Lagos hadi Kigali ndoto ya Afrika yatimia

Ukuaji wa Kiuchumi

Eneo la biashara huru limeridhiwa hii leo na hivyo kutoa fursa kwa nchi za Afrika kuimarisha biashara baina yao na hivyo kukuza siyo tu uchumi bali pia maisha ya kijamii ya wakazi wake.

Nchi za Afrika zimeridhia azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani himo na hivyo kuhitimisha harakati za miaka zaidi ya 40 tangu tamko la utekelezaji la Lagos la kutaka kuwa na eneo kama hilo.

Zaidi ya marais na naibu marais 19 wameshiriki kwenye utiaji saini wa azimio hilo mjini Kigali, Rwanda baada ya kikao kisicho cha kawaida cha viongozi wa Muungano wa Afrika, AU.

Akizungumza na Priscilla Lecomte, wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika, ECA mjini humo, Ali Mufuruki ambaye ni Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa kundi la kampuni za Infotech nchini Tanzania, amezungumzia mambo muhimu ya kufanikisha makubaliano hayo.

Viongozi wa Muungano wa Afrika, AU, wakisaini azimio la Kigali la kuanzisha eneo la biashara huru barani Afrika, AfCFTA, hii leo tarehe 21 Machi 2018 mjini Kigali nchini Rwanda.
ECA
Viongozi wa Muungano wa Afrika, AU, wakisaini azimio la Kigali la kuanzisha eneo la biashara huru barani Afrika, AfCFTA, hii leo tarehe 21 Machi 2018 mjini Kigali nchini Rwanda.

(Sauti ya Ali Mufuruki)

Akaenda mbali zaidi kuzungumzia umuhimu wa nishati katika kufanikisha makubaliano hayo..

(Sauti ya Ali Mufuruki)

Baadhi ya viongozi wa Afrika wametia saini itifaki ya watu kutembea huru barani humo, itifaki ambayo itawezesha waafrika kupata hati ya kusafiria ya Afrika.