Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauritania fanyeni uchaguzi kwa amani: Guterres 

katibu Mkuu António Guterres mbele ya waandishi habari , makao makuu ya UN
UN Photo/Mark Garten)
katibu Mkuu António Guterres mbele ya waandishi habari , makao makuu ya UN

Mauritania fanyeni uchaguzi kwa amani: Guterres 

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umojaa wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa vyama vyote nchini Mauritania kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa njia ya amani na unakuwa wa kuaminika.

 

 

Watu wa taifa hilo leo wanapiga kura kuchagua wabunge, viongozi wa majimbo na manispaa. 

Katika taarifa iliyotolewana msemajiwake, Bwana Guterres amesema anafuatilia kwa karibu maendeleo ya 

uchaguzi wa taifa hilola Afrika Magharibi. 

Katibu Mkuu amezitaka pande zote kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na kuruhusu ushiriki 

wa wadau wote. 

Ametoa wito kwa pande zote “kuhakikisha utawala wa sheria unaheshimiwa na kwamba haki za binadamu za raia wote wa Mauritania zinazingatiwa". 

Kwa mujibu wa duru za habari vyama 98 vya kisiasa vinashiriki kwenye uchaguzi wa mwaka huu ikiwa ni 

ongezeko kubwa ukilinganisha na uchaguzi uliopita.