Pongezi Mauritania kwa uchaguzi wa amani:Guterres

 Pia Mauritania ilifanikisha zoezi la kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wakimbizi kutoka Mali waliozaliwa  katika kambi ya Mbera
UNHCR
Pia Mauritania ilifanikisha zoezi la kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wakimbizi kutoka Mali waliozaliwa katika kambi ya Mbera

Pongezi Mauritania kwa uchaguzi wa amani:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres, amewapongeza watu wa Mauritania na serikali yao kwa kufanya uchaguzi wa bunge, mikoa na manispaa kwa amani nchini humo

Uchaguzi huo uliofanyika  tarehe mosi mwezi Septemba ulishuhudia ushiriki mkubwa wa vyama vya siasa na wannchi waliojitokeza kupiga kura..

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu anahimiza vyama vyote kuendeleakukumbatia hali ya amani amani wakati na baada ya kutangazwa kwa matokeo. Pia amewasihi viongozi wa kisiasa na wagombea kutatua migogoro na tofauti zao kupitia mazungumzo na kwa mujibu wa sheria.