IOM yazindua mpango mpya wa kuimarisha uwezo wa Afrika Magharibi kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaopotea
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) leo tarehe 4 mwezi Novemba mwaka 2025, limezindua mpango wa kihistoria kwa kushirikiana na serikali za Gambia na Mauritania, wenye lengo la kuimarisha uwezo wa kitaifa katika kukabiliana na vifo na kupotea kwa wahamiaji wanaosafiri kwenye njia zinazounganisha bara la Afrika na Ulaya.