Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atoa wito kwa viongozi na raia kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani Msumbiji

Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi akiwa na wanafunzi mara baada ya mkutano wa kimataifa wa wahisani kwa ajili ya nchi yake.
@UN Msumbiji

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anfuatilia kwa karibu hali nchini Msumbiji kfuatia uchaguzi mkuu uliofanika tarehe 15 mwezi huu wa Oktoba.

Bwana Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ijumaa jioni amesema Msumbiji imetoka mbali katika juhudi zake za kujenga amani ikizingatiwa pia makubaliano ya amani yaliyotiliwa saini hivi majuzi.

Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akisema kwamba uchaguzi wa hivi karibunu ni hatua muhimu katika mchakato wa demokrasia wa nchi hiyo.

Halikadhalika bwana Guterres ametoa wito kwa watu wa Msumbiji, ikiwemo viongozi wa kisiasa katika tabaka mbali mbali na wafuasi wao, kuendelea kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuendeleza amani na utulivu wakati huu muhimu katika historia ya nchi hiyo.