Pongezi Mauritania kwa uchaguzi wa amani:Guterres

katibu Mkuu António Guterres mbele ya waandishi habari , makao makuu ya UN
UN Photo/Mark Garten)
katibu Mkuu António Guterres mbele ya waandishi habari , makao makuu ya UN

Pongezi Mauritania kwa uchaguzi wa amani:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres, amewapongeza watu wa Mauritania na serikali yao kwa kufanya uchaguzi wa bunge, mikoa na manispaa kwa amani nchini humo.

Uchaguzi huo uliofanyika  tarehe mosi mwezi Septemba ulishuhudia ushiriki mkubwa wa vyama vya siasa na wannchi waliojitokeza kupiga kura..

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu anahimiza vyama vyote kuendelea kukumbatia hali ya amani amani wakati na baada ya kutangazwa kwa matokeo. Pia amewasihi viongozi wa kisiasa na wagombea kutatua migogoro na tofauti zao kupitia mazungumzo na kwa mujibu wa sheria.